TATO: YAIOMBA SERIKALI KUONDOA KODI ZISIZO ZA LAZIMA.

Mwenyekiti wa Karibu Fair Sam Dian



Joseph Mwema Mtunza (TATO)

Chama cha Mawakala wa Utalii Tanzania TATO (Tanzania Association of Tour Operators)  kimewataka wamiliki wote wa makampuni ya Utalii ambao hawajajisajili kwenye chama hicho wafanye hivyo ili waweze kushirikiana katika mambo mbalimbali pamoja nakutatua changamoto zitakazo jitokeza.

Hayo yamesemwa na ndugu Joseph Mwema ambaye pia ni muweka hazina wa chama hicho kuwa chama hicho ni kikongwe cha Utalii hapa nchini ,watu wengi wenye makampuni hawakielewi maana wengine wapo mahali ambapo hapana wawakilishi sawia, na ndani yao wapo wanaofanya kazi kinyemela.

Aidha Mwema amesema kuwa ili mtu awe mwanachama  wa Tato lazima awe na leseni ya biashara ambayo nabinatambulika,pia Tato inaisaidia serikali kuangalia watu wanaofanya biashara bila kibali na kutoa taarifa,hivyo ni vyema kama  mtu ana kampuni ya Utalii ajisajili ili atambulike.

Amesema kuwa kazi kubwa ya Tato ni Utetezi na ushawishi, kufanya mazingira ya biashara yawe rafiki kwa kwa kila mwanachama, kuwa msemaji wa wafanyabiashara ya Utalii kwa serikali, hivyo basi bila kuwa mwanachama hayo mambo ya msingi huwezi kuyapata,maana hili ni jukwaa linalowakutanisha watu wote wenye makampuni ya Utalii wanyama na vivutio pamoja na Utamaduni.

Sambamba na hayo (TATO ) imeiomba serikali ya Tanzania kuwajengea mazingira rafiki na salama,ikiwemo kodi ambazo zinagongana, iangalie kodi ambazo ni muhimu ziendelee kusalia na zile ambazo siyo muhimu ziondolewe.


Viongozi wa TATO pamoja na Mwenyekiti na muandaaji wa maonyesho ya Karibu Fair wakiwa katika picha ya pamoja. Wa kwakza kushoto ni Michael Mollel,wa pili kulia ni ndugu Sam Dian ambaye ni mwenyekiti wa Karibufair,anayefuata ndugu Joseph Mwema (TATO)  na wa mwisho ni ndugu Vito Sakaya (TATO)

Mwenyekiti wa Karibu fair ndugu Sam Dian aliyesimama akizungumza na wageni katika maonyesho,pamoja na ndugu Joseph Mwema (TATO) aliyechuchumaa alizungumza na mteja wake.


Sambamba na hayo mwenyekiti wa Karibufair ndugu Sam Dian ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tanzania Travel Safari Company,amesema kuwa karibufair imeshafanya maonyesho 17 ambayo yameweza kuwaunganisha wadau wa utalii kutoka Afrika na dunia nzima kuja kwenye vivutio vya asili Tanzania na kukutana namaopereta wa kuwahudumia wageni.

Amesema kuwa maonyesho Karibufair wameweza kushiriki makampuni 300 kutoka Afrika Mashariki,Jamuhuri ya watu wa China ,Ujerumani ,Uingereza,Ubelijiji ,na Ulaya Mashariki.

"Tunaiomba serikali itupatie maeneo ya kudumu ya kufanyia maonyesho haya kwani maeneo tuliyonayo kwa sasa siyo ya kudumu,tunatumia Magereza ground Arusha, na tunaiomba serikali iongeze bajeti katika wizara husika  kusapoti maonyesho kama haya kadhalika iwekeze nguvu za kutosha katika Masoko mapya ya Utalii duniani,ambayo hayajafahamika mfano;Urusi ,Australia,na Maeneo mengine ili kuvumbua masoko mengine alisema Sam."

Sam amesisitiza kuwa makampuni ambayo hayakupata nafasi yakushiriki katika maonyesho ya Karibufair 2016 ambayo yalifanyika hivi karibuni Magereza ground Jijini Arusha,amesema tayari ofisi zimeshafunguliwa kuanzia tarehe 26-28 mei 2017 Magereza ground Arusha kwa kujiandikisha.

No comments