MADIWANI WEKENI KANDO SIASA.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Francis Miti akizungumza na Madiwani wa Halmashauri hiyo katika kikao kilichofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa halamashauri hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya mfuo wa jimbo ,ni Diwani wa kata ya
Makamu mwenyekiti wa Madiwani ndugu Edward L.Mbapai,ambaye pia ni diwani wa kata ya Naalarami,akiwa anawasilisha taarifa ya maendeleo katika Kata hiyo kwenye baraza la madiwani.
Afisa Elimu wa Halmashauri ya Monduli Bi.Theresia Kyara akiwa katika baraza hilo ili kuchabua maswala ya shule zilizopo katika Halmashauri hiyo,na kutoa majibu ya maswali yaliyoulizwa.
Diwani wa kata ya Selela Cathbert Meena,akiwa katika baraza la madiwani katika halmashauri ya Monduli,ambaye alitaka kufahamu kuhusu utatuzi wa kero ya wanyama pori kudhuru mifugo ikiwemo mbuzi,pamoja na kondoo,jambo ambalo mkuu wa wilaya hiyo alimwagiza Afisa wanyama pori Silvanus Mawanja,afuatilie na aandike takwimu upya na zenye usahihi,kwani ya kwanza ilionekana imekosewa.
Picha tofauti tofauti za madiwani wakiwa wamesimama baada ya kuimba wimbo wa Taifa ,wakiwa wanasikiliza dua ikiwa inasomwa mna mwenyekiti wa halmashauri ,ndugu Isack J.Capriano,baada ya hapo kila diwani alipewa maelekezo ya kikao kilichofanyika kwa siku mbili.
Madiwani wametakiwa kuweka kando itikadi za vyama vyao,wafanye kazi kwa manufaa ya wananchi wa Monduli, huku wakifahamu kuwa kila jambo wanalolifanya ni kwaajili ya Wanamonduli.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa halmashauri ya Monduli ndugu Isack J. Capriano katika baraza la madiwani lililofanyika kwa siku mbili kwenye halmashauri hiyo na kuwasihi kuwa waache siasa ,baliwaangalie masuala ya maendeleo ya wananchi,wasimamie vijiji pamoja na kulinda mali ya halmashauri hiyo.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa lengo kuu la baraza hilo ni kupokea taarifa za maendeleo kutoka kwenye Kata na vijiji ili kuona namna ya kuondokana na changamoto kwenye Kata hizo pamoja na kujadili mairadi iliyochelewa kutekelezwa kutokana na uchaguzi kuwa itaanza kutekelezwa.
Aidha katika kikao.hicho cha madiwani wamekubaliana kukutana tarehe 15 june 2016,ili kujadili mgogoro uliopo kwenye eneo la Jeshi na malisho ,wahusika watakuwa viongozi wote wa vijiji 17,pamoja na wataalam watakutana Kata ya Arkatani saa tano kamili asubuhi.
Sambamba na hilo madiwani hao wamemuomba mkurugenzi wa halmashauri hiyo,kuwandalia semina walau ya siku mbili ili waweze kuelewa na kujifunza sheria na kanuni za uendeshaji wa baraza la madiwani.
Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Monduli Godfrey Luguma, akifuatilia kwa makini hoja zilizokuwa zikichambuliwa katika baraza la madiwani wa halmashari hiyo.
Madiwani wakiwa tayari kuingia ukumbini kwenye baraza la madiwani katika halmashauri ya Monduli.
No comments