Polisi yanasa Bunduki zilizokuwa zikitoroshwa Tabora
Polisi Mkoani Tabora imekamata bunduki nne zilizokuwa zinatoroshwa ikiwa ni
siku kadhaa baada ya Mkuu wa mkoa wa Tabora, Agrey Mwanri, kutoa wiki
moja kwa ajili ya wanaomiliki silaha mkoani humo kuzisalimisha kwa hiyari.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora,
Kamishna Msaidizi wa Polisi Khamis Selemani Issa, amesema silaha hizo
zilikuwa zinatoroshwa kutoka wilaya ya Kaliua kwenda maeneo mengine baada
ya amri ya mkuu wa mkoa.
Kamanda Issa amesema kuwa kati ya waliokamatwa ni pamoja na mtoto wa
miaka 16 hiyo jeshi la polisi linachunguza kwa kina juu ya umri halisi ya
mtuhumiwa huyo aweze kufunguliwa mashtaka kutokana na umri wake.
Kamanda huyo wa Mkoa wa Tabora ameendelea kuwasihi wananchi
wanaomiliki silaha kinyume cha sheria Mkoani humo kuendelea kuzisalimisha
kwa hiari na kusisitiza endapo mtu atakutwa katika opresheni ya kuzisaka
silaha hizo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

No comments