VETA&AIRTEL: WAMEANZA KUTOA MAFUNZO KWA NJIA YA SIMU.

Bi Hawa Bayumi Meneja Huduma za Jamii kutoka Airtel Dar es salaam.
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Veta Kilichopo Kipawa Jijini Dar es salaam,Mhandisi Lucius Lutenganya.
Mkuu wa Chuo cha VETA kilichopo Oljoro Jijini Arusha,Ndugu Banga Deusdedit Mrefu.
Meneja masoko wa Kanda Airtel Brightone Majwala 
Kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Msadizi Utawala Arusha akisalimiana na Mkuu wa chuo cha VETA,Mhandisi Lucius Lutenganya  walipokutana Jijini Arusha  kwenye kutoa Elimu kuhusiana na Mafunzo ya ufundi kwa njia ya simu uliowezeshwa kwa ushirikiano wa Airtel na VETA.
Kutoka kushoto Meneja Masoko wa Kanda Brightone Majwala ,akiwa na Meneja Huduma za Jamii Bi Hawa Bayumi wakiwa wanatoa elimu kwa wananchi wa Arusha kuhusiana na VSOMO,yaani mfumo wa mafunzo ya ufundi kwa njia ya simu.
Mratibu wa Mradi wa VSOMO Tanzania ndugu Gosbert Kakiziba kutoka VETA Kipawa Jijini Dar es salaam.

Mkuu wa Chuo cha VETA Oljoro Arusha akitoa elimu ya VSOMO pamoja na kujibu maswali mbalimbali aliyoulizwa.na baadhi ya wananchi na madereva Bodaboda maeneo ya Mountmeru Jijini Arusha
Mratibu mradi wa VSOMO Tanzania ndugu Gozbert Kakiziba kutoka Veta Kipawa Jijini Dar es salaam akiwa.anawaelekeza baadhi ya vijana namna ya kujiunga na Vsomo kupitia simu zao za mkononi yaani smartphone ya android
Kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Utawala Arusha ndugu Mushashu Analet ,Mkuu wa Chuo VETA Kipawa  Mhandisi Lucius Lutenganya ,akifuatiwa na Mkuu wa chuo cha VETA kilichopo Oljoro Arusha ndugu Banga Deusdedit Mrefu pamoja na Mratibu Mradi wa Vsomo Tanzania Ndugu Gosbert Kakiziba .
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Arusha wakifuatilia kwa makini elimu inayotolewa kuhusiana na mfumo wa mafunzo ya ufundi kwa njia ya simu yaani VSOMO yaliyokuwa ikiendelea kutolewa.
Wakazi wa Arusha wakifuatilia na kusoma vipeperushi vya Vsomo walivyopewa maeneo ya Mountmeru Jijini Arusha kuhusu mafunzo ya ufundi kwa njia ya simu.
Mkuu wa chuo cha VETA Kipwa Jijini Dar  es salaam,Mhandisi Lucius Lutenganya akimsaidia kijana huyo pichani kuelewa maana ya VSOMO Jjini Arusha.


ARUSHA
Chuo cha Ufundi Veta kwa kushirikiana na kampuni ya mawasiliano ya Airtel wamezindua mfumo wa mafunzo ya ufundi kwa njia ya simu ujulikanao kama VSOMO ambapo mwanafunzi anasoma kwa kutumia simu yake ya mkononi ya smartphone ya android.

Akizungumza katika ufunguzi huo Mkuu wa chuo cha VETA kilichopo Kipawa jijini Dar es salaam Mhandisi Lucius Lutenganya amesema kuwa VSOMO ni mfumo wa mafunzo ya Ufundi stadi kwa njia ya simu uliowezeshwa kwa ushirikiano wa Airtel na VETA.

Lucius amesema kuwa mfumo huo utamsaidia mwanafunzi kusoma mahali popote atakapo kuwepo kwa muda mfupi akiwa na simu ya smartphone,kisha atapatiwa mtihani wakufanya akifaulu vizuri anapatiwa cheti cha ufaulu kutoka VETA.

Kwa upande wake Meneja Huduma za Jamii bi Hawa Bayumi amesema kuwa namna ya kujiunga na VSOMO ni kwa kutumia smartphone ya android,unapakua App ya VSOMO kupitia google play store na unajisajili bure.

Bi Hawa ameainisha kuwa gharama za kujiunga na VSOMO kwa kila kozi  ni Tsh.120,000/= na mwanafunzi atalipia kupitia airtel money kwa kupiga *150*60# anakuwa tayari ameshalipa na anaanza masomo yake bila usumbufu wowote.

Naye Mratibu Mradi wa VSOMO ndugu Gosbert Kakiziba amesema kuwa hadi sasa kozi walizoanza nazo ni pamoja na Ufundi pikipiki( bodaboda) Ufundi wa umeme wa majumbani,Ufundi wa simu za mikononi,Ufundi wa Alluminium ,Utaalamu wa masuala ya urembo pamoja na ufundi wa kuchomelea vyuma.

Gosbert amesema kuwa baada ya mwanafunzi kusoma kwa njia ya simu kisha kupewa mtihani,wao VETA wanamchukua mwanafunzi huyu ili kujiridhisha  na kukaa nae chuoni kwa wiki mbili akipatiwa mafunzo kwa njia ya vitendo baada ya hapo muhitimu huyu atakabidhiwa cheti na mamlaka ya ufundi stadi nchini VETA.

Naye Meneja Masoko wa Kanda kutoka Airtel ndugu Brightone Majwala amesema kuwa hadi sasa tayari wameshafikia mikoa mitano ya Tanzania, kuhusiana na mfumo huu wa mafunzo ya ufundi kwa njia ya simu na wanatarajia ifikapo desemba mwaka huu watakuwa wameshafikia mikoa ishirini hapa mchini.

Brightone amesema ili uweze kupata mafunzo ya ufundi kwa njia ya simu ya mkononi itampasa mwanafunzi awe line ya airtel vinginevyo ataikosa fursa hiyo.


No comments