Ajali ya EgyptAir kisanduku kuchunguzwa
Wataalam wa masuala ya anga wamefanikiwa kurekebisha kifaa kinachotunza
kumbukumbu ya mwenendo wa ndege cha EgyptAir iliyoanguka mwezi uliopita
na kuua watu 66 waliokuwamo ndani yake.
Hatua hiyo inawapa nafasi wachunguzi hao kuweza kuzitafakari na kuzifuatialia
taarifa zitakazobainisha ni kwanini ndege hiyo ilianguka mashariki mwa bahari
ya Mediterranian.
Taarifa rasmi kuhusiana na uchunguzi huo zinasema kuwa
kazi ya kusikiliza na kuzifuatilia sauti hizo itafanyika ndani ya saa chache
zijazo. Kisanduku hicho cha mawasiliano kimefikishwa mjini Paris Ufaransa jana
jumatatu kutoka Cairo Misri ambapo kimepelekwa huko ili kuondoa tabaka za
chumvi zilizokizunguka chombo hicho.
Hata hivyo kinatarajiwa kurejeshwa katika maabara za mjini Cairo kwa uchunguzi zaidi baada ya marekebisho yotekukamilika ,mapema wanasheria nchini Ufaransa walifungua kesi ya mauaji
dhidi ya ajali hiyo kwa madai kuwa ilitokana na hujuma. Wanasema hakuna
uthibitisho wowote kuwa ajali hiyo ilitokana na ugaidi
Habari hii ni kwa mujibu wa BBC.
No comments