MITI:MADIWANI FICHUENI MIRADI HEWA ILIYOJIFICHA.


Mkuu wa Wilaya ya Monduli Francis Miti.

Madiwani wametakiwa kufuatilia rasilimali zilizopo katika halmashauri hiyo,kwani kwa kufanya hivyo itawasaidia kubaini miradi hewa iliyopo ,ukizingatia fedha za miradi ya maendeleo katika kila kijiji zinakuja mwezi julai mwaka huu.

Hayo yanesemwa na mkuu wa wilaya ya Monduli Francis Miti alipokuwa akizungumza na madiwani wa halmashauri hiyo katika baraza la madiwani lililokuwa kwa siku mbili kwani ni vyema wakawa makini.kufuatilia na kutambua miradi hewa katika kata na vijiji ili waweze kuitambua miradibhewa inayoharibu maendeleo ya Monduli.

Aidha mkuu huyo amewataka wananchi wa monduli wanaoishi kwenye kata,Wilaya,Mikoa na nchi mbalimbali, wajitoe kuchangia maendeleo ya wilaya hiyo,bila kusahau kuchangia madawati katika shule mbalimbali katika wilaya hiyo ili wanagunzi waweze kukaa na kusoma vizuri bila kupata usumbufu wowote.

Pia amesema kuwa katika wilaya ya Monduli ipo changamoto kubwa ya viongozi wa KIMILA wanaofahamika kama "LAIGUANANI"hawaelewani wamejigawa katika makundi,hivyo amewaagiza madiwani kuwaita viongozi hao ili waweze kuwasuluhisha waepushe mgogoro uliopo kati yao ili kuleta Amani katika jamii na wananchi wote kwa ujumla.



No comments