Alex Msama Amwangukia Mwakyembe Kumuomba Radhi Baada ya Gazeti ya DIRA Analolimiliki Kuchapisha Habari Zenye Utata
MFANYABIASHARA Alex Msama amemuomba radhi Waziri wa Sheria na Katiba,
Dk. Harrison Mwakyembe kufuatia habari mbili zilizochapishwa katika Gazeti la
Dira ya Mtanzania analolimiliki
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msama alisema
amejiridhisha kuwa habari hiyo iliyobeba kichwa cha habari ‘Utapeli wa
Mwakyembe wamwagwa hadharani’ haikufuata misingi ya uandishi wa habari.
Habari nyingine ambayo imeonekana kumchafua Dk Mwakyembe ni ile ya
Mwakyembe atuhumiwa kutapeli bilioni 2 ambazo zimemuumiza kiongozi huyo.
Alisema yeye kama mmiliki wa gazeti hilo amesikitishwa na habari hiyo na
kwamba hatua ya kwanza anayoichukua ni kumuomba radhi Waziri
Mwakyembe.
Msama alisema sambamba na kuomba radhi atamfikishia barua Mwakyembe
ya kumtaka radhi kwa tukio hilo.
“Nimesikitishwa na habari hii kwa kuwa haikuzingatia misingi ya uandishi wa
habari, ilihukumu na kuonyesha kuwa lengo lake lilikuwa kumharibia jina Waziri
Mwakyembe, ninachukua nafasi hii kumuomba radhi nikiwa mmiliki wa gazeti
hilo,” alisema Msama.
Aidha Msama alisema hatua nyingine anayochukua ni kumsimamisha kazi
mhariri wa gazeti hilo, Mussa Mkama kwa kuwa alishindwa kufanya kazi yake
kwa umakini ya kuhakikisha habari anazozipitisha zinafuata misingi ya uandishi
wa habari na weledi.
Alisema Mkama alipaswa kuhakikisha anafuata weledi lakini alishindwa kufanya
hivyo kwa hiyo anamsimamisha kazi na kwamba hatua nyingine kali za
kinidhamu zitafuata.
“Mimi ni mfanyabiashara sijui mambo ya uandishi, nilimuajiri nikiamini
atasimamia yale aliyofundishwa chuoni, kwa kuwa ameshindwa inabidi akae
pembeni kwanza,” alisisitiza Msama.
Ameahidi kuwa katika Gazeti la Dira ya Mtanzania litakalotoka Juni 27, kwa
ukubwa uleule atamuomba radhi Waziri Mwakyembe.
Hivi karibuni Waziri Mwakyembe aliitisha mkutano wa waandishi wa habari
mjini Dodoma akilalamikia kuwa habari mbili za gazeti hilo iliyochapishwa na
Gazeti la Dira ya Mtanzania la Juni 20 na la Juni 23 mwaka huu zililenga
kumchafua na kuahidi kuwa atalishtaki kupitia habari hizo mbili.bbnzjsisjsnbbn
No comments