Mlipuko wa bomu wawaua watu 18 Somalia


Habari kutoka Somalia zinasema kuwa watu 18 wameuawa baada ya bomu
kulipuka na kuharibu kabisa basi walimokuwa wakisafiria katika mji mkuu wa
Somalia, Mogadishu.

Bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara lililipua gari lililokuwa limewabeba
abiria. Wote waliouawa walikuwa raia.

Mashambulizi hayo yalitokea katika mji wa karibu wa Lafole.
Inadhaniwa kuwa washambuliaji hao walikuwa wakilenga gari la wanajeshi
lililokuwa karibu.
Mara kwa mara wapiganaji wa Al Shaabab hulenga wanajeshi wa Serikali.

Habari hii ni kwa mujibu wa BBC.








No comments