Dkt. Mabofu:waingiza magari wasiyotumia mawakala kuingia matatani Na Vero Ignatus
| Dkt,Egid Mabofu, Kaimu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya viwango ( TBS) nchini Tanzania.
Vero Ignatus Arusha .
Wanunuzi wa magari kutoka nchi za nje pasipokupitia kwa
mawakala walio na ubia na nchi ya Tanzania kuingia matatani.
Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Viwango nchini Tanzania Dkt.Egid Mabofu kwenye mkutano wa wadau
uliokutanisha taasisi mbalimbali zinazojihusisha na viwango amesema ikiwa
mnunuzi wa gari ataliingiza gari lake nchini bila kupitia kwa wakala
watanyang'anywa magari hayo na kuyaharibu au kuyarudisha yalipotoka .
Ameainisha
nchi za wakala wa uingizaji wa magari nchini alisema ni Uingereza
,Japani ,Dubai ambazo kama magari yatapitia kutoka nchi hizo sheria
hazitaweza kuwabana wanunuzi hao
Amesema kuwa lengo la kufanya hivyo ,ni kuthibiti uharibifu wa mazingira utokanayo
na matumizi ya bidhaa duni zisizokuwa na viwango nchini .
Awali
amesema, matumizi ya bidhaa duni yamechochea uharibifu wa mazingira na
kusababisha kuwepo na madhara makubwa ya uharibifu wa mazingira pamoja
na watu
Pia amesema ,kama shirika bado
linakabiliwa na changamoto ya umuhimu wa matumizi wa bidhaa bora kwa
walaji na kusababisha kuwepo kwa kwa ongezeko la uzalishaji wa bidhaa
duni nchini
"Tunataka walaji au watumiaji wawe
wa kwanza kukataa bidha duni ,tunajua wakikataa wao basi mtengenezaji
atajirekebisha '"alisema Kaimu mkurugenzi
Meneja
wa shirika la Mazingira nchini , Clara Makenya ,alisema kama shirika
wamejipanga kuhakikisha hadi ifikapo 2030 wameweza kuthibiti mazingira
kupitia matumizi endelevu ya bidhaa zenye viwango nchini
Dkt.Egid Mabofu amesema ,uharibifu wa mazingira pamoja na kuzagaa kwa takataka kwenye
jamii inatokana na utumiaji wa bidhaa duni zinazopelekea kutupwa
kiholela mitaani.
"Huwezi kununua bidhaa iliyo
na kiwango kizuri ukatupa ,kwanza kuisha kazi ,bidha feki ama zisizo na
kiwango ni lazima zitupwe kwakua hazikai kwa muda mrefu ,"alisema Clara
Pia
alisisitiza kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya mazingira na viwango vya
bidhaa nchini hivyo alisema kama shirika wamejikita katika kuhakikisha
kunakuwepo kwa bidhaa zilizo na viwango ili kupunguza uharibifu wa
mazingira
Meneja wa Viwango nchini ,Mary Meela
ambaye pia ni mratibu wa mradi wa utekelezaji wa viwango ,alisema
kwasasa kupitia mradi huo wanajianda kutunga sera ambayo itaelekeza
udhitibi wa viwango vya bidhaa nchini
"Mpaka
sasa hatua sera za viwango ama sera za viwango vya chakula ,tunategemea
kuwa nazo kutokana na ukutanishaji wa wadau mbalimbali juu ya udhitibi
wa viwango nchini,"alisema Mary Meela.
|
No comments