Godwin Mollel:Serikali iruhusu soko huria la uuzwaji madawa

Na Vero Ignatus Arusha

 Licha ya kuzuka kwa sintofahamu kuhusu kuwepo kwa uhaba wa dawa za binadamu nchini, Waziri kivuli wa Afya na Mbunge wa Siha Godwin Mollel, ameitaka serikali iruhusu soko uria la uuzwaji wa madawa nchini

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, ameshauri serikali iruhusu shirika la Bohari la dawa nchini liwekewe mshindani wake ili kuwezesha kuwepo kwa uwajibikaji na utendaji bora wa usambazaji wa dawa nchini
Awali alisema shirika hilo licha ya kuwa linaidai serikali bado liko nyuma katika utoaji wa huduma zake 

"leo si ajabu ukaandikiwa dawa na ukakosa hospitali za serikali ama kwenye phamasia, "alisema Godwin
"MSD imekuwa kero mahospitalini, vifaa tiba wanavyotoa si imara," alisema Godwin 

Aidha alitaka serikali itoe majibu kwa serikali kuwa ni kwanini nchi ya Tanzania inanunua dawa peke India na si kenya ambako ni nchi karibu na Tanzania 

Pia akifafanua juu ya ununuzi wa dawa alisema nchi ya Tanzania imekuwa ikitegemea kununua dawa nchi ya India peke huku ikisababisha kutumia muda mrefu kuingiza dawa nchini 

"Kwanini tunaagiza dawa India na Si Kenya kama Kenya dawa hizo hizo zinapatikana , alisema Mbunge
"Tumegundua kuna ufisadi mkubwa unaofanyika nchi ya India ndio mana dawa zinanunuliwa India pekee 

Pia alisema kutokana na upungufungu wa dawa nchini serikali irudie pendekezo la kambi rasmi bungeni kuhusu kuongeza bajeti ya dawa kutoka 6.1 bilioni hadi 295 bilioni 

Katibu wa chadema Kanda ya Kaskazini Amani Golugwa, amesema uhaba wa dawa nchini umekuwa ni kero kubwa hasa kwa Wazee ambao ndio waathirika wakubwa wa tatizo hilo 

"Tumetembelea wazee wa mkoa wa Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Manawa, kilio cha wazee ni dawa, wazee wakienda mahospitalini wanaishi kupewa paracetamol, panadol na magnesium, hali ni mbaya sana, "alisema Amani

Kutokana na kuwepo kwa changamoto ya utekelezaji wa mpango kabambe wa Arusha" Arusha City Master plan "wilaya ya Arusha, Arumeru na Arusha jiji wamekubali kuungana na kuwa pamoja kutekeleza mradi huo 

Awali mradi huo ambao haukuwa sawa kwenye wilaya hizo kupitia mkutano huo wa waandishi wa habari, wilaya hizo zimekubali kutoa tofauti zao ili kuendeleza mkoa wa Arusha 

Mwenyekiti wa halmashauri ya Arumeru, Wile Njau alisema wilaya hizo zimeweka makubaliano ya pamoja kubainisha miradi ambayo haikuwekwa kwenye mpango mji, ikiwa pia ni kuunganisha miradi hiyo pamoja kwaajili ya maendeleo ya mkoa wa Arusha. 

Pia alisema wamekubaliana kuanzisha kamati ya pamoja ya kusimamia mpango kabambe wa Arusha City Master Plan

No comments