MAJONZI
na vilio vilitawala ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda wakati Kijna Said Mrisho anayedaiwa kujeruhiwa na kutobolewa
macho na Salumu Henjelewe maarufu kama Scorpion Buguruni Sheli alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari mbele ya mkuu wa mkoa Dar es Salaam
leo asubuhi kuwa hata ona tena katika maisha yake kufuatia kujeruhiwa
vibaya kwenye mishipa ya macho na mtuhumiwa huyo na kupoteza uwezekano
wa kuona.
Mrisho
alisema anamshukuru sana Rais John Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda kwa jitihada walizofanya za kumsaidia kupata
matibabu lakini imeshindika kwa kuwa mishipa yote yenye uwezo wa
kumfanya aweze kuona imeharibiwa vibaya na mtuhumiwa huyo hivyo ataweza
kuona tena katika maisha yake."Iwapo
kama mishipa isingeharibiwa kwa visu mama yangu kipenzi Halima Lwiza
Abdallah alikuwa yupo tayari kutoa jicho lake moja kwa ajili ya
kunisaidia niweze kuona lakini kwa bahati mbaya hilo halitawezekana
baada ya madaktari kunieleza kuwa mishipa ya macho yangu imeharibiwa"
alisema Mrisho kwa huzuni na kuanza kulia.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda amesema wamepokea kwa huzuni taarifa hiyo ya madaktari na
kumuomba Mrisho asikate tamaa kwani serikali itaangalia jinsi ya
kumsaidia.Makonda alisema serikali itatoa sh.milioni 10 kama mtaji ili
ziweze kumsaidia wakati wakiangalia namna ya kuwashirikisha watu
wengine kwa ajili ya kumsaidiaMakonda alisema serikali itamsaidia
kufanyiwa upasuaji wa kuwekewa macho ya bandia ili awe katika mwonekano
wa kawaida ingawa hatakuwa haoni."Pamoja na kumpatia kiasi hicho cha
fedha katika kipindi hiki cha mpito ambacho atakuwa akihitaji kwenda
katika matibabu na sehemu zingine tutakuwa tukimsaidia usafari wa kwenda
maeneo hayo" alisema Makonda. |
No comments