Burundi kujiondoa mahakama ya ICC


Mamia ya watu wameuawa tangu kuanza kwa machafuko Aprili mwaka jana
Baraza la Mawaziri nchini Burundi, kwa kauli moja limeidhinisha mswada wa kuliondoa taifa hilo kutoka kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC.

Serikali ya nchi hiyo tayari imewasilisha mswada huo bungeni ambapo unatarajiwa kujadiliwa na hatimaye kuidhinishwa.

Makamu wa rais Gaston Sindimwo amesema serikali ya Burundi haiogopi kutengwa zaidi na jamii ya kimataifa.

"Wajua, huenda tukatengwa. Lakini ni sawa mradi tu tuwe tunajivunia uhuru wetu. Ni nchi ngapi hazijajiunga na mahakama hii? Zimetengwa? Kuna Marekani, Urusi, Uchina na nyingine nyingi na kun ahata mataifa jirani hapa ambayo hayajajiunga na mahakama hiyo," alisema.

"Lakini bado yameendelea kuwepo. Hatufanyi chochote kibaya. Ni haki yetu kujitoa mahakama ya ICC. Ni uamuzi wetu; mswada sasa umewasilishwa bungeni. Tuko tayari kwa matokeo yoyote."

 Zaidi ya watu 400 wameuawa kwenye machafuko yaliyotokea tangu rais Pierre Nkurunziza aamue kuwania urais kwa muhula wa tatu Aprili mwaka wa 2015. Wengine 200,000 wametorokea mataifa jirani wakihofia 
Wafuasi wa serikali na wale wa upinzani pia wamekuwa wakiuawa mara kwa mara katika mashambulizi ya kulipiza kisasi.usalama wao.

Chanzo BBC.




Rais Nkurunziza akiapishwa kwa muhula wa tatu Agosti mwaka 2015

No comments