TRA WAVUKA MALENGO YA UKUSANYAJI MAPATO ARUSHA.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Mkoani Arusha (TRA)Apili Mbaruku akiwa ofisini kwake.Picha na Vero Ignatus Blog.
|
Na Vero Ignatus Arusha.
Mamalaka
hiyo imekusanya shilingi bilioni 64.6, ikiwa imevuka malengo yake iliyojiwekea
awali ya kuweza kukusanya shilingi bilioni 63.1.
Ongezeko
hilo, ni sawa na asilimia 102, kulingana na meneja wa Mamlaka ya mapato (TRA) mkoani Arusha, bwana
Apili Mbaruku.
Akizungumza
katika mahojiano maalumu na blogu hii, bwana Mbaruku alielezea kuwa ongezeko
hilo linatokana na majumuisho ya makusanyo ya mwezi Julai na Agosti mwaka huu.
“Ni kweli
tumeweza kukusanya kiasi hichi cha fedha, nahii inatokana na kukua kwa mwamko
wa ulipaji kodi mkoani hapa japokuwa bado zipo changamoto kadhaa za baadhi ya
wafanyabisahara kutokuelewa umuhimu wa kulipa kodi,” alisema meneja huyo.
Apili
ametaja sekta ya utalii kuongoza katika ulipaji huo wa kodi.
“Tumekuwa
tukitoa elimu kwa wafanyabiashara waweze kuelewa umuhimu wa kulipa kodi na
kukwepa usumbufu usio na lazima,” alishauri meneja huyo.
Hata hivyo,
Mbaruku aliweka wazi kuwa ofisi yake ilishindwa kufikia malengo ya ukusanyi wa
mapato kwa mwaka wa fedha 2015/16.
“Kwa mwaka
uliopita malengo yetu yalikuwa kukusanya shilingi 329.5 lakini kwa bahati mbaya
tulipata shilingi bilioni 324.6 tu”.
Akifanunua
zaidi kuhusu makusanyo ya mwaka huu,
Mbaruku alisema kuwa kiasi cha bilioni 30.3 zilitokana na makusanyo ya ndani wakati
shilingi bilioni sita zilitokana na malipo ya ushuru.
Aidha,
Mbaruku ameongeza kuwa ofisi yake inatarajia kukutana na maofisa wa jiji la
Arusha kuanza kukusanya makusanyo ya kodi za majengo.
Kulingana na meneja huyo wa TRA, ofisi yake inalenga kukusanya kodi kutoka kwenye majengo 20,
536 mkoani hapa. Mamlaka ya mapato mkoni Arusha(TRA) imevuka lengo la
makusanyo yake kwa mwaka wa fedha 2016/17.
“Nia yetu ni
kuanza kukusanya kodi kutoka kwenye majengo hayo, na tayari tumeshafanya
mawasiliano na maofisa wa jiji na kuweza kubainisha majengo hayo,” aliongeza meneja huyo wa TRA mkoani Arusha.
No comments