MSHAMA:ENEO LA LULANZI LISIENDELEZWE KWANZA.


KIBAHA PWANI
Image result for assumpta mshama
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Asumpter Kibaha.


MKUU wa wilaya ya Kibaha mkoani Pwani Asumpter Mshama amewataka wananchi walioko kwenye eneo la Lulanzi wilayani maarufu kama Matunda kutoendeleza eneo hilo hadi pale atapoomba Rais ababidlishe matumizi kutoka viwanda hadi makazi.

Ameyasema hayo mjini Kibaha alipofanya mkutano na wananchi walio kwenye eneo hilo ambalo awali lilitengwa kwa ajili ya viwanda lakini lilirudishwa kwa Halmashauri ya Mji baada ya wamiliki kushindwa kuendeleza kwa kujenga viwanda.

Mshama amesema kuwa kutokana na hali ambayo ilijitokeza hapo na wananchi kujenga makazi huku Halmashauri ikiwataka waondoke kwani matumizi yake bado hayajabadilishwa kuwa makazi ya kuishi.

“Kuwabomolea wananchi itakuwa ni kuwaonea kwani wametumia gharama kubwa itakuwa ni kuwaonea ni vema tukamshauri Rais abadilishe matumizi ya eneo hili na kuwa makazi kwani kwa wakati ule madhumini yalikuwa ni hayo lakini kutokana na wamiliki kushindwa kujenga viwanda na watu tayari washajenga ni vema tukaomba yawe makazi kuliko kubomoa,” alisema Mshama.

Amesema kuwa nyumba zilizojengwa katika eno hilo ni 150 na watu wamewekeza itakuwa siyo busara kuwabomolea kwani hata Halmashauri ya Mji wa Kibaha ilifanya makosa kwa kuwaacha watu kujenga hadi kufikia idadi kubwa kiasi hicho.

Aidha amewataka watu ambao wana viwanja na hawajajenga kutokujenga au kufanya maendelezo yoyote hadi pale majibu yatakapopatikana na wale waliojenga waendelee kusihi hapo hadi mwezi Novemba ambapo atakuwa amewasiliana na wizara husika kuhusiana na eneo hilo

Kwa upande wake ofisa mipango miji wa Halmashauri ya Mji Kibaha Gili Simiyu alisema kuwa eneo hilo lilipitishwa kuwa sehemu ya viwanda tangu mwaka 1980 na hakuna mabadiliko yaliyofanyika yakufanya kuwa eneo la makazi.

Simiyu alisema kuwa watu waliojenga hapo walijenga kimakosa na watu waliowauzia hawakustahili kufanya hivyo kwani eneo hilo lilikuwa ni maalumu kwa ajili ya viwanda tangu miaka ya 80 na hadi sasa bado matumizi yake hayajabadilishwa.

Amesema kuwa baada ya mji huo kuwa Halmashauri ya Mji Mdogo mwaka 2005 walianza kufanya mchakato wa eneo hilo kuwa kitovu cha Mji baada ya waliopewa kwa ajili ya kuanzisha viwanda ksuhindwa kufanya hivyo ilikabidhiwa Halmashauri ambapoviwanja 101 vina hati huku 37 vilikuwa bado havijasajiliwa na Rais ndiye mwenye uwezo wa kutengua matumizi eneo hilo.

No comments