Warembo 30 kutoka mikoa mbalimbali watakaoshiriki miss Tanzania wawasili Arusha


Warembo 30 wanaoshiriki kinyanganyiro cha kumsala Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara tu baada ya kutembelea ofisi za gazeti la Guardian zilizopo ndani ya mkoa wa Arusha
  Baadhi ya warembo akiwemo mwenyeji wao ambaye ni miss Arusha wa pili kulia Maurine Ayubu wakiwa  ndani ya ofisi za gazeti la Gurdian na Nipashe zilizopo jiji Arusha
Warembo wakisikiliza kwa makini jambo linalowahusu mara tu walipowasili ofisini hapo
Msimamizi wa kituo cha Gazeti la  Gurdian  na Nipashe mkoa wa Arusha na Manyara  Edward Qorro akiwa anatoa maelekezo mafupi kwa warembo juu ya kazi zinazofanya na magazeti hayo katika mkoa huu

 Msimamizi wa kituo cha Gazeti la  Gurdian  na Nipashe mkoa wa Arusha na Manyara  Edward Qorro akipokea mkoa wa Shukrani kutoka kwa Mshiriki wa mashindano ya miss Tanzania kutoka mkoa wa Arusha Maurine Ayubu ambaye pia ndio mshindi wa Miss kanda ya kaskazini mara baada yakumaliza kutmbelea ofisi za magazeti hayo zilizopo apa Arusha
 
 Mkuu wa kituo akatumia fursa hiyo na warembo hao kujipatia picha ya kumbukumbu

Meneja masoko wa gazeti la Gurdiaan   Swalehe Walii akiwa anatoa zawadi ya soda kwa mrembo Maurine Ayubu ambaye ni mwenyeji wa warembo wenzake wanaoshiriki shindano hilo kwani ametokea mkoa wa Arusha 
Warembo wakiwa katika picha ya pamoja walipotembelea ofisi za guardian na Nipashe jijini Arusha
 warembo wakiwa wanatoka katika ofisi za gazeti la  The gurdian mara baada ya kumaliza kutembelea  

Alexander Nikitas ambaye ni muandaaji wa miss Tanzania Kanda ya Mashariki
Albert Makoye pichani ambaye ni mkuu wa Kambi ya Miss Tanzania nchini  akifanya Amahojiano na  mwandishi habari za michezo Bertha Mollel
Moureen Ayubu Mollel ambaye ni miss Arusha na miss Kanda ya Kaskazini akiwa ndiye mwenyeji wa wawembo wenzie mkoani hapa maana ni mzaliwa wa Arusha.
Na Vero Ignatus Arusha.

 Warembo 30  kutoka mikoa mbalimbali  hapa nchi ni wanashiriki shindano la kumsaka mrembo wa Tanzania (Miss Tanzania) wameingia Rasmi mkoani Arusha na kutembelea ofisi za gazeti la The Guardian na Nipashe  ikiwa ni moja ya kazi ambazo watazifanya wakiwa mkoani hapa.
Akizumza na waandishi wa habari  Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania Albert Makoye alisema kuwa wameingia jijini hapa leo na wanakaa kwa muda wa siku tatu ,na katika siku hizo wanampango wa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii
Aidha alisema kuwa pia ndani ya siku hizo tatu kutakuwa nashindano la Top model ambalo litafanyika Jumamosi October 15 katika ukumbi wa Triple A ulipo ndani ya jiji la Arusha 
"tunafanya shindano hilo katika ukumbi wa triple A natunarajia wananchi wengi wa Arusha watajitokeza kuwaona warembo hawa na kiingilio cha shindano hilo ni shilingi 10000 tu hivyo napenda kutumia mda huu kuwaalika wananchi wa Arusha kuja kumuangalia nani atakuwa Top Model"alisema Makoye
Alisema kuwa  mbali na hapa warembo hao wameshatembelea mikoa mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Dodoma,Singinda ,Dar  es Salaam  hapa Arusha na hatimaye wanatarajia kuondoka na kwenda mwanza ambapo ndipo shindano hili linafayanyika kwa mwaka huu .
Alisema kuwa shindano la Miss Tanzania linatarajiwa kufanyika october 29 katika ukumbi wa Rock City Mall  ambapo alibainisha adi sasa warembo wote 30 wapo vizuri na wanasubiria siku yenye ifike na maandalizi yashindano yamekamilika
Kwa upande wake mkuu wa kituoa cha The Gardian /Nipashe mkoa wa Arusha na Manyara Edward Qorro alitoa shukrani kwa warembo hao kuwatambelea na kuwatakia kila la kheri katika mashandano hayo wanayotarajia kushiriki hivi karibuni.

No comments