Dawa ya mpango wa uzazi kwa wanaume
| Dawa mpya ya mpango wa uzazi kwa wanaume |
Dawa inayotolewa kwa njiya ya
sindano imetajwa kama mafanikio makubwa ya njiya ya mpango wa uzazi
miongoni mwa wanaume.Watafiti kutoka Marekani wamesema dawa hiyo
imefikia asili mia 96 ya mafanikio baada ya kufanyiwa majaribio miongoni
mwa wanaume 270.
Wataalamu hao wamekua wakitafuta jinsi ya kupunguza idadi ya manii bila kusababisha madhara ya uzazi. Kimaumbile wanaume hutoa manii kila wakati na wanasayansi wamekua wakitaka kupunguza idadi kutoka milioni 15 hadi milioni moja.
Baadhi walisema iliwachukua mwaka mmoja kabla ya idadi kamili na inayotakikana kurudi. Baadhi ya madhara kama vile mfadhaiko, usununu, vipele usoni na maumivu ya misuli yalisababisha wanaume 20 kujitoa kwenye utafiti. Mtafiti mkuu wa dawa hii Dkt. Festin amesema wanaangazia njiya nyingine ya kuboresha dawa hiyo ikiwemo kuiotoa kama mafuta.
No comments