RC ARUSHA :KAULI ZA RAIS ZISIPOTOSHWE.



 
Image result for mrisho gambo
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo
 


Na Vero Ignatus Arusha.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,amewataka wananchi na madiwani kutopotosha kauli ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli,kuhusu wamachinga wafanye kazi zao bila kubughudhi  huku akiwataka  kujikita katika kufuata utaratibu na sheria juu ya mipango miji

Hayo ameyasema wakati akimjibu mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema kwenye mkutano wa RCC ambapo mbunge huyo alisema mkoa wa Arusha umeharibiwa na Kauli ya Magufuli,iliyopelekea kuzagaa kwa wamachinga na gereji bubu

Gambo amesema kauli ya rais haikuwa yenye lengo la kuharibu mipango miji ila ilikuwa na maana nzuri  iliyokuwa na lengo la kuboresha maisha ya Watanzania ,hivyo warudie kusoma tena hotuba ya rais ili waweze kuelewa vizuri.

Amewataka viongozi wa upinzani wanaompinga yeye wasome vizuri alama za nyakati na hatakuwa tayari kumnvumilia yeyote yule atakayejitokeza kuyumbisha kazi zake aewataka kufanya kazi kwa kufuata kanuni na sheria zinavyoagiza na wafanye kazi za wananchi maana ndilo jambo la muhimu kuliko kuingia kwenye malumbano.
lema
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema

Awali  akizungumza mbunge lema wa Arusha mjini amesema kuwa hali ya sasa ya jiji la Arusha ni mbaya kutokana na kutokana  na kukithiri wimbi la wamachinga kwenye maeneo yasiyorasmi huku jiji kuonekana kuchafuka.

"Mhe,mkuu wa mkoa Arusha kwa sasa imekuwa ile ya miaka 10 iliyopita mji umeharibika si masokoni,barabarani,pamejaa watu yaani hapeleweki,kwa vile mji huu umeharibika sisi tumeamua kutokuhudhuria vikao mpaka hapo tutakapoonana na uongozi wa juu watusaidie maana maazimio ya mipango mji siyo haya mji umeingiliwa "alisema Lema


Nae Mstahiki  Meya wa Jiji la Arusha Calist Lazaro amesema kabla ya raisi kusema kauli hiyo baraza la madiwani lilifanuikiwa kuwahamisha wamachinga na gereji bubu zote mjini na kuzitafutia maeneo yao lakini karibia wote wamerudi mjini.
"Mji umechafuka kwasasa hata masokoni hawatoi tena ushuru tunaomba rais Magufuli atusidie kutatua hili"alisema Meya.
Image result for kalisti lazaro
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Kalist Lazaro




No comments