Kifo cha muuza samaki chazua maandamano Morocco
Maelfu wa raia wa Morocco walifanya
maandamano wikendi hii katika miji kadhaa baada ya muuza samaki mmoja
kukanyagwa hadi kufa na lori la kubeba takataka alipokuwa akijaribu
kuchukua samaki wake ambao alikuwa amepokonywa na maafisa wa polisi.
Kifo chake kinafananishwa na kile cha muuza matunda wa Tunisia mwaka 2010 ambacho kilisababisha maandamano makubwa.
Mfalme wa Morocco King Mohammed VI amewaagiza maafisa wake kutembelea familia ya Fikri.
Wizara ya maswala ya ndani pamoja na ile ya Haki zimeahidi kuanzisha uchunguzi
No comments