Mwanamuziki nguli wa Kenya Achieng Abura afariki dunia
Kwa mujibu wa The Standard, amefariki Alhamis hii kwenye hospitali ya taifa ya Kenyatta jijini Nairobi. Bi. Abura alikuwa amelazwa katika wodi binafsi akitibiwa ugonjwa ambao haujajulikana.
Bi. Abura Alifariki dunia mida ya saa 12 jioni. Mapema mwezi huu, muimbaji huyo aliandika kuwa afya yake si nzuri na madaktari walimshauri aongeze uzito kisha kuupunguza kupitia mazoezi.
Chanzo cha karibu na familia yake kilidai kuwa alihamishwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi baada ya hali yake kuwa mbaya.
Wasanii mbalimbali wa Kenya wametuma salamu zao za rambirambi kupitia mitandao ya kijamii.
No comments