Rais Buhari: Mke wangu ni wa kwangu jikoni
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari
amejibu onyo kutoka kwa mkewe ambaye alikuwa ametahadharisha kwamba
hatamuunga mkono uchaguzi mkuu ujao iwapo hatafanya mabadiliko serikali.
Bw Buhari kwa sasa yumo kwenye ziara rasmi nchini Ujerumani na kwa mujibu wa shirika la habari la AP, amemjibu mkewe wakati wa kikao cha wanahabari akiwa pamoja na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel.
Bw Buhari anaanza kwa kucheka kidogo kisha kusema: "Sijui mke wangu ni wa chama gani, lakini najua yeye ni wa kwangu jikoni na sebuleni na chumba hicho kingine."
Amesema alijaribu kwa miaka 12 kuwa rais na akafanikiwa kwa mara ya nne.
"Kwa hivyo, nina ujuzi kushinda yeye na watu wengine wa upinzani, kwa sababu mwishowe nilifanikiwa. Si rahisi kuridhisha vyama vyote vya upinzani nchini Nigeria au kushiriki serikalini."
Bi Merkel alionekana kushangazwa na matamshi ya Buhari
No comments