LEMA AZUA KASHESHE KWENYE UZINDUZI WA HOSPITAL YA MAMA NA MTOTO JIJINI ARUSHA.
| Baadhi ya wananchi waliohudhuria uzinduzi wa ujenzi wa hospitali ya mama na mtoto ambaye jina lake halikufahamika mara moja akimsihi mbunge Lema wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema atulize jazba shughuli hiyo ya uzinduzi iendelee na ampe mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo nafasi aendelee na hotuba yake kwa wananchi waliohudhuria. |
| Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akiwa anatulizwa na mchungaji Wilfred Mlay ,Wa kwanza kushoto ni mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa anatulizwa na mfadhili wa Mradi huo ambaye ni daktari bigwa wa magonjwa ya kina mama na Mtoto Duniani Edrew Brown |
Na.Vero Ignatus Arusha.
Wakati Mzozano
ukiendelea kati ya Mbunge Lema na Mkuu wa mkoa Mrisho Gambo,umepelekea
wafadhili wa ujenzi wa mradi wa Mama na Mtoto kutoa machozi mbele ya
wananchi kutokana na kitendo kilichotokea
Awali ,Mtendaji mkuu wa mradi wa wakunga afrika ,Dr Andrew Blowin amesikitika kutokea kwa kitendo hicho kilichopelekea kuvurugika kwa uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa hospitali ya Mama na mtoto na kusema hakutegemea kama ingefikia hatua hiyo
"Tulitaka siku hii iwe yenye furaha kwa Mama na Mtoto lakini tunasikitika imekuwa si siku ya baraka juu ya kuanzisha mradi huu,"alisema Dr.Adrew
Awali ,Mtendaji mkuu wa mradi wa wakunga afrika ,Dr Andrew Blowin amesikitika kutokea kwa kitendo hicho kilichopelekea kuvurugika kwa uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa hospitali ya Mama na mtoto na kusema hakutegemea kama ingefikia hatua hiyo
"Tulitaka siku hii iwe yenye furaha kwa Mama na Mtoto lakini tunasikitika imekuwa si siku ya baraka juu ya kuanzisha mradi huu,"alisema Dr.Adrew
Mkuu wa mkoa kugoma kuja kwenye Uzinduzi
Uzinduzi
wa mkutano ulikuwa uanze saa 4:30 asubuhi lakini Mkuu wa Mkoa Mrisho
gambo alikaidi kuja na kusema hatoweza kufika kama Mbunge wa Mjini
Godbless Lema atakuwepo
Kuzozana
huko kulianza mpaka Mbunge Lema alipoamua kumigia katibu mkuu Kijazi na
kumuambia kuhusu mkuu huyo wa mkoa kughahiri kwenda kwenye uzinduzi huo
wa mradi wa mama mtoto
Baada
ya simu hiyo kupigiwa katibu mkuu ,Mkuu wa Mkoa Mrisho gambo alifika
kwenye eneo la tukio saa 7 mchana na kuanza kuongea na wananchi
Kulipoanza Mabishano
Baada
ya mkuu huyo kufika na kuanza kuongea na wananchi ,Mrisho hambo alianza
kuelezea kuhusu mradi huo na kusema mradi huo ulikuwa unaendeshwa na
Taasisi ya Ukunga ya Afrika "Maternity Africa"na eneo ambalo lilitakiwa
kujenga hospitali hiyo ya Mama na Mtoto lilitolewa na Marehemu Nyaga
Mawala ,hivyo eneo hilo lilikuwa na Mawala
Lakini ia alisema eneo hilo halikuwa na taasisi ya ARDF hivyo alitaka siasa ziache kutumika kutokana na eneo hilo linawahusika
Lema alivyoanza kumjibu
Kutokana
na mkuu huyo kuongea hivyo ,Mbunge huyo alianza kugomba na kusema mkuu
huyo anapotosha umma kwakua eneo hilo lilitolewa chini ya uzimamizi wake
na ufadhili aliuangaikia yeye mwenyewe
"Mkuu wa Mkoa anaongea uongo"aache uongo ,"mimi nimeangaika kupata hili eneo na kupata ufadhili,"alisema Lema
"Nimegundua anataka kutufifisha upinzani ,tunajua katumwa kufanya hivi na hatutakubali ,"alisema Lema
Kuhusu
mradi huo ,Mtendaji mkuu wa mradi wa Ukunga Afrika ,amesema mradi huu
umepanga kuboresha huduma ya Mama na mtoto na kuhakikisha wanaumaliza
ugonjwa wa Festula
ambapo kupitia mradi huu watawezesha kutoa mafunzo ya ukunga
yatatolewa kwa wanafunzi ikiwa lengo ni kupambana na matatizo ya uzazi
kwa mama na mtoto kbala hajajifungua na baada ya kujifungua.
Amesema mradi huo utagharimu kaisi cha shilingi 9 bilioni lengo ikiwa
kuhakikisha maswala yatokanayo na uzazi yanatokomea Tanzania ,ambapo fedha za mradi huo zinatoka kwenye taasisi ikishirikiana na watu binafsi wanaotoa michango yao kutoka nje ya nchi .
"Tunatazamia
mradi huu utatibu maelfu ya kina mama na zitakuwa bure ,pia wanatoa
msaada yao ni watu waliokuwa na upendo na nchi hii ,"alisema Dr.Adrew.
No comments