Bendera: Tanzania na Korea Kaskazini zazozana
Taifa la Tanzania limefutilia mbali
usajili wa meli kadhaa za Korea Kaskazini kwa kupeperusha bendera za
taifa hilo kinyume na sheria.
Hatahivyo hakutoa idadi kamili ya meli hizo.
''Meli za Korea Kaskazini zilipigwa marufuku na Umoja wa Mataifa na hazikuruhusiwa kusafiri ama hata kutia nanga'',alisema Mahiga.
''Kwa hivyo meli hizi zimekuwa zikijaribu kutafuta njia kukiuka vikwazo hivyo ili kuweza kuendelea na biashara zao,na mbinu moja ni kupeperusha bendera za mataifa tofauti''.
Waziri huyo amesema kuwa malalamishi yametumwa katika serikali ya Korea Kaskazini wakilaumu biashara hiyo ya ujanja.
''Shirika la kimataifa la maswala ya baharini pia limeelezewa ili kuwakamata wamiliki wa meli hizo'',aliongezea Mahiga.
No comments