NGUZA VIKICNG NA MTOTO WAKE PAPI KOCHA KUTUMBUIZA WAFUNGWA WENZAO GEREZANI KESHO LIVE!!
MWANAMUZIKI nguli wa dansi Nguza Vicking “Babu Seya” na mwanaye Papy
Kocha ambao wanatumikia kifungo gereza la Ukonga, watapanda jukwaani Ijumaa hii
na kumwaga uhondo ‘live’ kwa wafungwa wenzao.
Hiyo ni katika tamasha maalum la wafungwa lililoandaliwa na Global
Publishers katika kuadhimisha siku ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere –
“Nyerere Day”.
Mratibu wa tamasha hilo, Juma Mbizo amethibirtishia kuwa
vibali na taratibu zote za shughuli hiyo itakayofanyika ndani ya gereza la
Ukonga jijini Dar es Salaam, zimekamilika.
Mbizo amesema mbali ya Papy na Nguza kutumbuiza, pia kutakuwa na
burudani kutoka kwa The African Stars “Twanga Pepeta” na Msagasumu.
Kwa mujibu wa mbizo, tamasha hilo litakuwa na michezo mbali mbali kwa
wafungwa kama vile mechi za mpira wa miguu, kuvuta kamba, kukimbia na magunia,
pamoja na kuimba na kurap ambapo zawadi mbali mbali zitatolewa kwa washindi.

No comments