SERIKALI:IPO TAYARI KUSAIDIA MACHINJIO ARUSHA
Na Vero Ignatus Arusha
Serikali imesema iko tayari kusaidia machinjo ya mifugo ya Arusha meat ,kuanzisha kiwanda cha kuchakata ngozi ili kusaidia kuinua pato la taifa
Akizungumza
hayo alipoenda kutembelea Machinjio hayo kuangalia shughuli
mbalimblai zinazofanywa na machinjio hayo ,Naibu waziri wa Mifugo ,Uvuvi
na Ufugaji Wiliam Ole Nasha,alisema serikali ipo tayari kusaidia
machinjio hiyo kuanzisha kiwanda hicho ilikuwezesha kukuza soko la ajira
nchini
Pia imesema
itazungumza na mifuko ya hifadhi ya jamii nchini ili iweze kuwekeza
katika kiwanda hicho ambacho kitatoa ajira nyingi kwa vijana.
“Serikali ya awamu ya tano inatoa msukumo mkubwa wa kuwekeza kwenye viwanda has wa vinatumia malighafi "alisema Ole Nasha
"Naomba
kuanzia sasa muangalie namna ya kujenga kiwanda cha kuchakata ngozi
inayotokana na mifugo mnayoyanjiacha hapa kwa kuwa mna eneo kubwa la
kutosha ambalo halitumiki”
Naibu
waziri huyo ,pia alitoa ushauri kwa uongozi wa machinjo hayo kuangalia
namna ya kutengeneza vyakula vya kuku kupitia kuchakata mifupa na damu
za mifugo
Pia
amesema, ilisoko la walaji liongezeke ipo wajibu kwa machinjio hayo
kuangalia namna ya kuongeza thamani ya nyama kwa walaji wake
Kwa
mujibu wa Ole Nasha Tanzania ni nchi ya pili katika bara la Afrika kwa
wingi wa mifugo lakini haina viwanda vya kuchakata ngozi na kwamba
ngozi inayotumika katika gereza la Karanga liliko mkoa wa Kilimanjaro
inatoka nchini Kenya.
Hata
hivyo ,amesema kanda ya kaskazini imekuwa ikipoteza mapato yake
yatokanayo na uuzwaji wa mifugo hiyo huku mifugo mingi ikiuzwa nchini
kenya
Upande
wa kaimu meneja wa Arusha Meat,Joseph Singuya amesema machinjio hiyo
ina uwezo wa kuchinja ng’ombe kati ya 400 mpka 500 kwa siku lakini
kutokana na wilaya ya Arumeru iliyopo jirani na eneo hilo wanachinja
ng’ombe 140 na mbuzi 130
No comments