RC.Gambo awataka wananchi kuchangia (CHF)
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Mashaka Gambo alip[otembelea katika kijiji cha Engaresoro ,baada ya kusikiliza changamoto mbalimbali wanazopitia na kuwachangia bati 200 kwaajili ya ujenzi wa nchumba cha upasuaji wa kituo cha afya kijijini hapo Engaresoro.
|
Wananchi wa kijiji Engaresero,wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa
Arusha,Mrisho Mashaka Gambo (hayupo pichani),alipofanya ziara katika kijiji
hicho ambapo amewasisikitiza wananchi wa Engaresero
kuchangia mfuko wa bima ya afya(CHF)
ilizipatikane fedha kwaajili yakununua vifaa tiba katika kituo hicho cha afya.
Na.Vero Ignatus Arusha
Kutokana na changamoto
nyingi zinazoikumba sekta ya afya
hususani kwenye Zahanati na Vituo vya
afya mbalimbali hapa nchini ndio vinapelekea kuwa na huduma duni za kiafya.
Hayo yamesemwa na mkuu wamkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Ghambo alipotembelea katika kijiji hicho cha Engarosero na kuona changamoto wanayopitia wananchi hao haswa wakina mama na watoto wanaozaliwa.
.
“Mimi nitachangia mabati 200 kwaajili ya ujenzi wa
chumba hicho cha upasuaji na ninaomba wananchi mjitokeze kwa wingi katika
ujenzi wa chumba hicho ili tuweze kunusulu maisha ya kinamama na watoto
wanaozaliwa”.
Ukosefu wa vitendea kazi,upungufu wa watumishi wa
afya na ukosefu wa chumba chakujifungulia ndio changamoto zilizotolewa na
wakazi wa kijiji cha Engaresero Wilayani Ngorongoro.
Akitoa malalamiko hayo Bi.Omega Lemra alisema
wakinamama wengi wanapata shida sana wanapoenda kujifungua katika kituo cha
afya cha Engaresero kwasababu hakuna chumba cha upasuaji kwa wale wamama
wanaojifungua kwa upasuaji.
“Tumekuwa tukipata sana shida wakinamama ambao
tunaitaji kujifungua kwa upasuaji kwenye kituo chetu cha afya kwasababu hakuna
chumba cha upasuaji na hivyo kutulazimu kwenda Wilaya ya karibu ya Karatu
ambapo pia kuna umbali”,alisema Omega.
Aidha Gambo amewasisikitiza wananchi wa Engaresero
kuchangia mfuko wa bima ya afya(CHF)
ilizipatikane fedha kwaajili yakununua vifaa tiba katika kituo hicho cha afya.
Akifafanua zaidi juu ya upungufu wa watumishi wa
afya Mganga Mkuu wa Mkoa,Dokta Frida Mokiti,alisema halmashauri ya Ngorongoro
ipeleke maombi ya watumishi wa afya wanaoitajika katika kituo hicho nakuwaweka
katika bajeti ili waweze kuajiriwa mapema iwezekanavyo.
Mkuu huyo wa mkoa yupo katika ziara Wilayani Ngorongoro,ambapo anakutana na wananchi wa
vijiji mbalimbali nakusikiliza matatizo huku mangine yakipatiwa ufumbuzi na
mengine yakichukuliwa kwaufuatiliaji zaidi.
|
No comments