THURSDAY 30 MARCH 2016MWANAMKE MTANZANIA ANG'ARA KATIKA MASHINDANO YA KARATE KATIKA NCHI ZA AFRIKA YA MASHARIKI
Mwanadada Getrude Macha ameshika nafasi ya kwanza katika mchezo wa karate ambapo mashindano hayo yanajulikana kwa jina la (GOJUKAI) karate ya Afrika Mashariki yaliyofanyika nchini Uganda ambapo yamejumuisha nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi.
Rais wa chama cha GOJUKAI Karate Tanzania ambae pia ni Mkufuzi wa Gojukai Geofrey Cleodo Kalonga amesema kuwa,mchezo wa huu unamjenga mshiriki kiafya katika maisha yake yote, ambapo ameongeza kuwa mchezo huo hauna ukomo ukilinganisha na michezo mingine,kwani kadri umri unavyaozidi kuwa mkubwa ndipo mchezo unakuwa mkubwa zaidi.
Geofrey Kalonga amesema wao kwa ujumla wao kama chama cha Gojukai Karate Tanzania wanaiomba serikali wauruhusu mchezo huu uruhusiwe kuingia kwenye taasisi za elimu kuanzia shule za awali,shule za msingi, sekondari na vyuoni kwani ni taaluma inayofundisha nidhamu katika kiwango cha hali ya juu,pia inafundisha mbinu za kujihami.
Naye Rais wa shirikisho la West Coast Shotokan Karate Tanzania lililopo Jijini Arusha ,Bwana Dady Kassim Ramadhani, ameelekeza ombi lao kwa waziri wa habari, vijana utamaduni na michezo ,Mhe Nape Moses Nauye kutupia macho katika mchezo huo kwani ni karate inafundishwa katika majeshi mengu ,wameomba mchezo huo uthaminiwe kama inavyathaminiwa michezo mingine.
Amesema kuwa mchezo wa katate unatambulika Kimataifa ,ila wanasikitika kuwa.mchezo.huo hapa ndani yanchi hautambuliki hivyo wamemuomba Waziri mwenye dhamana kulitazama jambo hili kwa umakini kwani itakuwa faraja kubwa kwao.

No comments