Monday 25 April 2016 HISTORIA YA PAPA WEMBA

Habari kuwa mmoja wa vigogo wa muziki wa kiafrika Papa
Wemba ametutangulia mbele ya haki imepokewa kwa mshtuko
mkubwa na mashabiki wake kote duniani.

Video inayosambazwa katika mitandao ya kijamii inamuonesha
Papa Wemba akiendelea na kazi yake anayoifahamu zaidi ya
uimbaji kisha anaonekana akianguka ghafla jukwaani.
Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba 1949-2016.

Wanabendi wake waliokuwa jukwaani naye huko Abidjan katika
tamasha la muziki la #FEMUA wanaendelea kupiga densi tu
kabla ya mmoja wao kukimbia kumuokoa baada ya kuona
kasalia chini kwa sekunde kadhaa akiwa anatetemeka kisha
akazirai.

Shoo hiyo ya Papa Wemba ilikuwa moja katika mji mkuu wa
Ivory Coast Abidjan.
Msemaji wake Henry Christmas Mbuta Vokia, ameiambia Radio
Okapi kuwa
''Marehemu Papa Wemba alikuwa ameingia muda mchache tu
jukwaani kisha akacheza wimbo wa kwanza, mashabiki
wakamuomba awaimbie tena wimbo mwengine akakubali.

lakini dakika chache tu baada ya kuanza kupiga wimbo wa ke
wa tatu Papa Wemba alianguka na kuzirai ghafla jukwaani''
Watu wa shirika la msalaba mwekundu walijaribu kumsaidia
lakini hakuonesha dalili nzuru kwa hivyo wakampeleka
hospitalini kwa dharura lakini baada ya dakika karibu thelathini
hivi tukaambiwa kuwa Papa Wemba ametuacha''
Alisema Mbuta Vokia.

Msanii huyo nguli alikonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa
Soukus nchini DRC na kote duniani kwa kipaji chake cha
kipekee na sauti isiyokuwa na mfano.
Wengi waliitambua sauti hiyo ya na utunzi wake.
Alikuwa ni mtumbuizaji kamili.
Ni mweledi wa kuimba kucheza ala za muziki na pia kusakata
rhumba yaani kunengua kiuno.

Lakini je Papa wemba ni nani

Gwiji huyo wa muziki wa lingala alizaliwa mnamo Juni 14
mwaka 1949, katika eneo la Lubefu - Wilaya ya Sankuru nchini
Congo.
Jina lake halisi ni Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba.
Yeye alianza kazi ya muziki akiwa na umri mdogo mno.
Alikuwa akimfuata mamake katika matanga na hivyo akaibukia
kuwa mtunzi wa nyimbo za kuomboleza.
Alitunga wimbo wake wa kwanza "Madrigal" akiwa na umri wa
miaka
Shungu Wembadio alijiunga na kundi la ''Stukas'' kabla ya
kuliacha na kuunda kundi kubwa la Zaiko lana langa mwaka
huohuo wa 1969.
Zaiko Langalanga Sauti yake ya kipekee na uweledi wake
uliisaidia kundi hilo katika utunzi wa "Pauline", "Chouchouna",
"Liwa is somo".
Wemba wakati huo alijiunga na wanamuziki wenza wa Zaire
(Congo ilivyojulikana wakati huo) Nyoka Longo Jossart,
Manuaku Pepe Felly, Evoloko Lay Lay, Bimi Ombale, Teddy
Sukami, Zamuangana Enock, Mavuela Simeon, Clan Petrole
miongoni mwa wengine.

Wakati huo akianza Papa Wemba , jukwaaa la muziki nchini
humo lilikuwa limetawalwa na vigogo wa muziki Franco
Luambo wa TPOK Jazz, Tabu Ley Rochereau wa Afrisa, na
makundi mengine mapya kama vile Les Grands Maquisards, Le
Trio Madjesi, Bella-Bella, Thu Zaina na Empire Bakuba.
Hata hivyo sauti ya kipekee ya Papa Wemba akijulikana wakati
huo kwa majina yake kamili Jules Presley Shungu Wembadio
ilikonga mioyo ya wapenzi wa Soukus.
Kilele cha ufanisi wa kundi la Zaiko Langa Langa ulikuja miaka
ya mapema ya sabini.(1973)
Hapo ndipo Shungu alibadili jina lake na kuanza kuitwa jina la
utani ''Papa Wemba''.
Yolele

Miaka mitano baadaye aliihama kundi hilo na kujiunga na "Isifi
Lokole" hapo alitunga wimbo maarufu wa "Amazon", wimbo
aliokiri kumtungia mkewe.
Mwaka huo hakutulia lengo lake la kupambana na vigogo wa
muziki nchini Zaire haikuwa imekamilika.
Alijiunga na kundi lingine la "Yoka Lokole", kabla yake kuunda
kundi lake sasa la "Viva La Musica" mapema mwaka wa 1977.
Vibao vyake ni kama Mwasi,Show me the way, Yolele,
Mama,Proclamation"Chouchouna" (Papa Wemba), "Eluzam" na
" Mbeya Mbeya" (Evoloko Lay Lay), "BP ya Munu" (Efonge
Gina), "Mwana Wabi" , "Mizou" (Bimi Ombale) ,
"Zania" (Mavuela Somo. ,Emotion,Wake Up, Wake Up,Maria
Valencia, Le Voyageur,Rail On, Kaokokokorobo ,Legend

Jela
Papa Wemba aliwahi kukamatwa kwa madai ya ulanguzi wa
binadamu.
Tarehe 18 mwezi Februari 2003 maafisa wa idara ya upelelezi
nchini Ufaransa walimkamata Papa Wemba kwa tuhuma za
kuwaingiza raia wa Zaire (kama ilivyoitwa wakati huo DRC)
barani ulaya kinyume cha sheria.
Papa Wemba
Mahakama ya ubelgiji ilimpata na hatia mwezi Juni mwaka wa
2003 na ikamhukumu kifungo cha mwaka mmoja na miezi
mitatu jela.

Aidha mahakama hiyo ya Brussels ilimpiga faini ya euro
22,000.
Hata hivyo alitumikia kifungo cha miezi mitatu u nusu gerezani
baada ya mdhamini kulipia dhamana ya Euro €30,000.
Alipoachiwa huru aliwaambia mashabiki wake kuwa
aliyokumbana nayo akiwa gerezani yamemfunza mengi tu.
Katika utunzi wa wimbo wake "Numéro d'écrou" (2003)Papa
Wemba anasimulia kukutana na mwenyezi Mungu akiwa
gerezani.
Aidha anasema kuwa alibadilishwa mawazo na dini akitumikia
kifungo.

No comments