Sunday, April 24, 2016 Sad News: Mwanamuziki Nguli wa Congo Papa Wemba Afariki Dunia
Mwanamuziki nguli wa Congo Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba maarufu
kama Papa Wemba amefariki dunia huko Abidjan, Ivory Coast, usiku wa
kuamkia leo.
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema marehemu Papa Wemba amefia
hospitali alikokimbizwa mara baada ya kuanguka na kupoteza fahamu wakati
akiwa katika onesho jukwaani.
Papa Wemba alizaliwa June 14, 1949 huko Lubefu katika wilaya ya Sankuru
nchini Congo. Alijipatia umaarufu sana kwa sauti nyororo na midundo ya
Soukous ulimwenguni kote, ikiwamo Tanzania ambako amezuru mara kadhaa
na kujizolea mashabiki wengi
Papa Wemba alipoanguka na kupoteza fahamu katikai ya onesho
Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba maarufu kama Papa Wemba enzi za uhai wake.
Picha ikimuonyesha Papa Wemba akiwa amedondoka chini ndipo mauti ilipompata.
No comments