Rais mpya wa Ghana kuapishwa leo
Rais mpya wa Ghana
ataapishwa hii leo, katika taifa ambalo limetajwa na wengine kama lenye
kiwango bora zaidi cha Demokrasia Barani Afrika.
Kiongozi wa upinzani ashinda uchaguzi wa urais Ghana
Karibu viongozi 11 wa mataifa ya Afrika wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo, ambako hali ya usalama tayari imeimarishwa.
Baada ya kuapishwa kwake, viongozi wa Afrika watajadiliana jinsi ya kuhakikisha kuwa Rais wa Gambia Yahya Jamme anakubali kuwa alishindwa katika Uchaguzi Mkuu uliopita.
Chanzo bbc
No comments