MAONESHO YA ZANA ZA KILIMO YAFUNGULIWA KWA MARA YA KWANZA MKOANI ARUSHA

Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro ambaye amemuwakilisha muu wa mkoa katika ufunguzi wa maonesho hayo leo 26 januari 2016.picha na Vero Ignatus blog.



Mtaalamu wa Mawasiliano wa taasisi ya Agriculture Markets Development Trust(AMDT),Al-amani Mutarubukwa(kulia)akitoa maelezo kwa Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro(wa pili kulia)kuhusu taasisi hiyo inayowajengea uwezo wakulima katika mazao ya Ufuta na Mahindi katika mikoa mbalimbali nchini. 
Meneja wa Kampuni ya Monsanto nchini,Frank Wenga(kulia)akizungumza na wakulima waliofika kwenye maonesho hayo kujifunza mbinu za kilimo chenye tija. 
Wakulima kutoka maeneo mbalimbali wakipata elimu ya matumizi ya kilimo bora na chenye tija. Picha na Vero Ignatus Blog.
Wakulima wakipata maelezo kutoka kwa wataalamu namna ya kupata mazao bora .Picha na Vero Ignatus Blog.
Mmoja wa wakulima wakiangalia mazao yaliyostawisha kwa kufuata kanuni za kilimo katika maonyesho hayo leo 26 januari 2017.Picha na Vero Ignatus Blog.


 Na Vero Ignatus .Arusha.



Maonyesho ya zana za kilimo yamefunguliwa jijini Arusha ambapo ni mara ya kwanza yanafanyika katika viwanja vya Taasisi ya Utafiti wa kilimo ya Seliani iliyopo mkoani hapa na kushirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania



Mgeni rasmi katika maonyesho hayo ni mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro,ambapo amesema kuwa serikali inawashukuru wadau kwa kuupa mkoa wa Arusha heshima ya kufanyika kwa maonyesho hayo ambayo yatafanyika kwa muda wa siku mbili hivyo amewataka wananchi wajitokeze kwa wingi katika kujifunza teknolojia mpya za kilimo na ubunifu wa wataalamu mbalimbali .



Amewataka waonyeshaji kuangalia suala la bei kwani kwaasilimia 75-80 ya wakulima ni wakulima wadogowadogo hivyo ni vyema wakauza bidhaa zao kwa bei nafuu ili wakulima wa hali ya chini aweze kumudu kununua bidhaa ili waweze kuendana na kasi ya kilimo cha kisasa



Serikali kwa kushirikiana na wadau wa kilimo wanaangalia ni kwa namna gani
wataweza kuboresha sekta hii ya kilimo kwa kutoa elimu mbalimbali kwa wakulima ili kuepukana na kilimo duni ambacho kinasababisha hasara kwa wakulima nchini.



Mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa sekta ya kilimo inakabiliwa na changamoto wa ufugaji wa kiholele amabao hupelekea uharibifu wa mazingira,Teknolojia duni,ugumu wa kupata mitaji ya kuboresha miundombinu ya kilimo


Kwa upande wake mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Seliani amesema kuwa wamekua wakishirikiana na wadau mbalimbali wa kilimo ,katika uzalishaji wa Teknolojia ,pamoja na kuwatafutia wadau wa kilimo masoko ya mazao yao”Sisi Seliani tupo tayari kuwaunganisha wakulima na waonyeshaji wa teknologi utaongezeka pamoja na wakulima watafahamu namna ya kuhifadhi mazao yao baada ya uvunaji ili wasipoteze mazao kama ilivyokuwa kabla ya kupata elimu hiyo ya kilimo".

No comments