Jamaa aliyemtahiri mwanawe kwa kisu kortini Bunda
Moja ya
habari iliyoandikwa kwenye magazeti ya leo ni pamoja na hii ya kwenye
gazeti la Habari leo yenye kichwa cha habari ‘Amjeruhi vibaya mwanawe
kwa kumtahiri kwa kisu’
Gazeti
hilo limeripoti kuwa mkazi wa kijiji cha Mihingo wilayani Bunda mkoani
Mara, Marwa Elias amefikishwa mahakama ya wilaya ya Bunda kwa tuhuma ya
kumtahiri vibaya kwa kutumia kisu, kukata kipande kikubwa cha uume wa
mtoto na kumsababishia madhara makubwa mwilini mwake.
Kwa sasa mtoto anajisaidia haja ndogo kwa shida kutokana na kukatwa sehemu hiyo ya siri vibaya. Inadaiwa
baada ya tendo hilo mtuhumiwa huyo alitoweka na kwenda kwenye shughuli
zake akimuacha mtoto huyo akiwa kwenye hali hiyo, baadaye hivi karibuni
alikamatwa na kufikishwa polisi na kisha mahakamani.
Baada ya
kusomewa shitaka lake mtuhumiwa alikana kutenda kosa hilo na kupelekwa
mahabusu katika gereza la Nyasura nje kidogo ya mji wa Bunda, baada ya
kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
No comments