Yaliojiri Wakati wa Kutangazwa Mshindi wa Uchaguzi Mdogo Jimbo la Dimani Zanzibar.
Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa NEC Wilaya ya Magharibi Unguja
Bi Fatma Gharib akitangaza matokea ya Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Dimani
Zanzibar katika Ofisi za Tume zilioko katika Skuli ya Sekondari
Kiembesamaki Zanzibar baada ya kukamilika taratibu zote za Kisheria za
Uchaguzi na kupatikana mshindi wa Uchaguzi huo mdogo uliofanyika katika
jimbohilo baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbohilo Mhe Hafidh Ali Tahir
kufariki dunia mwaka jana.
Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi Ndg Ali Juma Ali, akiwa
katika ukumbi wa Tume ya Uchaguzi Skuli ya Sekondari ya Kiembesamaki
akifuatilia matekeo ya Uchaguzi Mdogo wa jimbo hilo la Dimani akiwa na
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Unguja Ndg Yussuf Mohammed
wakifuatilia matokeohayo.
Mshindi wa kinyanganyirocha kugombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa
Jimbola Dimani Ali Juma Ali akitia saini fomu ya matokeo baada ya
kutangazwa na tume kushinda uchaguzi huo.
Mshindi wa Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Dimani Zanzibar Ndg Ali Juma Ali akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi huo na kuwaahidi Wananchi wa Jimbo la Dimani kujiandaa na maendeleo ya jimbo lao na kuendeleza maendeleleoa yaliazishwa na marehemu Hafidh Ali Tahir
No comments