Shtaka linalomkabili mbunge wa Arusha mjini na mkewe kusikilizwa Februari 3 mwaka huu

Image result for picha ya lema na mkewe



Na.Vero Ignatus Arusha

Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema na mkewe Neema Lema wamefikishwa katoka mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Arusha kusomewa mashtaka yanayowakibili katika kesi namba 351 ambapo wanatuhumiwa kutuma meseji yenye ujumbe wa kumtukuna mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Mashaka Gambo

Wakili wa upande wa mshtaka Alice Mtenga amewataja mashahidi watano wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambao watatoa ushahidi katika kesi hii

Hata hivyo mawakili upande wa utetezi wakiongozwa na John Malya umetoa notisi ya pingamizi la awali la mdomo kuwa hati ya mashitaka ina mapungufu kwa hiyo baadae wataiomba mahakama itupilie mbali hati hiyo.

Hakimu anayesikiliza shitaka hili Nestory Barro ameiahrisha kesi hiyo hadi tareh 3 mwezi februari mwaka huu

No comments