KESI YA MKE WA BILLIONEA MSUYA YAENDELAE TENA LEO
DAR
ES SALAAM:
Maombi ya kufutiwa mashtaka yaliyowasilishwa kwenye Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini hapa na Miriam Msuya, mke wa aliyekuwa
bilionea mkubwa jijini Arusha, Erasto Msuya, leo yamesikilizwa
na kutolewa uamuzi mdogo mbele ya hakimu Mwambapa aliyesema jamhuri
ilikuwa na mamlaka ya kuiangalia hati ya mashtaka kabla haijaenda
mahakamani hapo, hivyo jamhuri ikapewa siku mbili kuiangalia upya hati
hiyo na hivyo kupangiwa Januari 11 mwaka huu kuwa siku ya kusikilizwa
tena.
Utetezi huo uliwasilishwa na wakili wa utetezi, Peter Kibatala,
anayemtetea mteja wake, Miriam Msuya, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya
kudaiwa kumuua mdogo wa marehemu Msuya, Anethe Msuya, Mei 25, mwaka
jana, Kigamboni jijini hapa.
Mshitakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Revocatus Muyela ambapo kupitia
kwa wakili wao, Kibatala ameiomba mahakama iwafutie mashitaka hayo kwa
kuwa hati ya mashitaka ina mapungufu na haionyeshi kama walikuwa na nia
ya kufanya uovu.
Mei 25, mwaka huu maeneo ya Kibada wilaya ya Kigamboni jijini Dar es
Salaam, Anethe aliuawa kwa kuchinjwa akiwa nyumbani Kibada. Wauaji
hawakuchukua kitu chochote kwenye nyumba hiyo. Bilionea Msuya aliuawa
Agosti, 2015 kwa kupigwa risasi. Cap: Miriam Msuya alipofikishwa
mahakamani Kisutu leo.

No comments