Maiti iliyozikwa Mbeya yakutwa nyumbani!
JIJI
la Mbeya limekumbwa na taharuki kwa siku mbili kutokana na tukio
lililojiri katika Mtaa wa Igoma A kata ya Isanga, la mwili wa mtoto
aliyekufa akiwa usingizini, kukutwa nyumbani baada ya wakazi wa mtaa huo
kutoka makaburini walikokwenda kuuzika.
Mwili uliozua gumzo jijini hapa na kusababisha wakazi katika kila kona kuuzungumzia, ni wa mtoto Haruna Kyando (9).
Kwa mujibu wa mashuhuda, tukio hilo lilitokea juzi ambako majira ya asubuhi wazazi wa mtoto huyo, waliamka na kukuta mtoto wao amefariki na kisha kuwajulisha ndugu, jamaa na marafiki juu ya msiba uliowakuta; ambao kama ilivyo kawaida kwa misiba yote watu mbalimbali walikusanyika wakiwemo majirani.Baada ya taratibu zote za kimsiba kufanyika, ulianza utaratibu wa kwenda kuuzika mwili huo katika makaburi ya zamani ya Isanga, ambayo kimsingi uongozi wa eneo hilo ulikwishapiga marufuku shughuli za maziko kwenye eneo hilo kutokana na kujaa na pia lina maji mengi.
Kilichowastaajabisha wakazi walioshiriki maziko hayo ni kuwa baada ya kutoka makaburini na kurejea nyumbani, waliukuta mwili wa marehemu ukiwa umelazwa kwenye godoro, kama ilivyokuwa awali kabla ya kuuingiza kwenye jeneza kwa ajili ya kwenda kuuzika.
Hapo ndipo ilipolazimu wananchi kurudi tena makaburini na kufukua kaburi na kukuta jeneza tupu likiwa halina mwili, hali iliyozusha maswali mengi, moja kati yake ikiwa ni nani aliyehakikisha kuwa mwili wa marehemu uliingizwa kwenye jeneza kabla ya kubebwa kwenda makaburini kuzika.
Kwa upande wake, wazazi wote wawili wa marehemu walisema wao hawakuelewa chochote kinachoendelea kutokana na majonzi ya mtoto wao, aliyefariki ghafla kwa ugonjwa wa kifafa.
Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Emmanuel Lukula alisema Januari 16, mwaka huu saa nne asubuhi katika Mtaa wa Igoma A, Kata ya Isanga Tarafa ya Sisimba, Polisi ilipokea taarifa kuwa maiti iliyokwenda kuzikwa katika makaburi ya zamani ya Isanga ilikutwa nyumbani, chumbani ikiwa kwenye godoro.
Kaimu Kamanda Lukula alisema kutokana na taarifa hiyo, Polisi walifuatilia na kubaini kuwa siku hiyo saa moja asubuhi, Jailo Kyando (36) ambaye ni muosha magari na mkewe Anna Elieza (32) wote wakazi wa Mtaa wa Igoma A, waliamka asubuhi na kukuta mtoto wao wa kwanza, Haruna Kyando (9) amefariki dunia akiwa amelala.
Alisema taarifa za awali zilieleza kuwa Haruna tangu utoto wake alikuwa na matatizo ya ugonjwa wa kifafa, hali iliyosababisha kubaki nyumbani pasipo kwenda shule kusoma.
Alisema kutokana na kifo hicho, msiba uliendeshwa na taratibu za mazishi zilifanyika ambako majira ya saa sita mchana jeneza lililetwa msibani na kuwekwa sebuleni kando ya mwili wa marehemu ambao ulikuwa umeviringishwa na blanketi na kulazwa chini kwenye godoro.
“Baada ya maombi yaliyoongozwa na waumini wa Kanisa la Kilokole Bonde la Baraka, vijana walibeba jeneza hadi makaburi ya zamani ya Isanga na kisha kuzikwa,” alieleza Kaimu Kamanda wa Polisi.
Alisema waombolezaji waliporudi nyumbani ndipo walitaharuki kuona mwili wa marehemu ukiwa chumbani umelazwa eneo ulipokuwa awali.
“Kutokana na hali hiyo, taarifa zilifikishwa Polisi mara moja, askari Polisi walifika na kurejesha hali ya amani kwa kuuchukua mwili wa marehemu ambao kwa sasa umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya. “Taratibu nyingine za mazishi zitafanyika leo (jana) tarehe 17.01.2017. Mpaka sasa bado haijafahamika ni uzembe /bahati mbaya wafiwa kusahau kuweka mwili wa marehemu kwenye jeneza au kulikuwa na hujuma zozote. Upelelezi unaendelea kuhusu tukio hili,” alibainisha Kaimu Kamanda.

WAKAZI JIJI LA MBEYA
WAFURIKA KUSHANGAA KABURI LILILOZIKWA JENEZA BILA MAITI
Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Mbeya wakiwa wamelizunguka kaburi
linalodaiwa kuzikwa jeneza bila mwili wa marehemu wakisubiri Jeshi la
Polisi kwa ajili ya kufukua kaburi ili kuhakikisha kama hakukuwa na
mwili wa marehemu.
Jeneza lililozikwa likifunuliwa kujua kama kuna maiti lakini la. (PICHA,
HABARI KWA HISANI YA MBEYA YETU BLOG
Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Mbeya wakiwa wamefurika kwenye makaburi ya
Isanga ambapo kuna kaburi linalodaiwa kuzikwa jeneza bila mwili wa
marehemu wakisubiri Jeshi la Polisi kwa ajili ya kufukua kaburi ili
kuhakikisha kama hakukuwa na mwili wa marehemu.Jeneza lililofukuliwa
likiwa halina kitu ndani yakeMwenyekiti wa Mtaa wa Igoma pamoja na Baba
wa Marehemu wakifunua jeneza kuhakikisha kama kulikuwa na mwili wa
marehemuVijana wakiwa wanaondoa jeneza makaburini na kulipeleka kituo
cha Polisi kwa ajili ya taratibu zingineJeneza baada ya kufukuliwa
kutoka kaburiniKazi ya Kufukua kaburi ikiendelea
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na matukio makubwa
ya uhalifu pamoja na wahalifu. Jitihada zinaendelea kwa kushirikiana na
wananchi kuhakikisha Mkoa wetu unakuwa mahala salama. Kumekuwa na tukio
01 la taarifa ya kifo kama ifuatavyo:-
Mnamo tarehe 16.01.2017 majira ya saa 10:30 Asubuhi huko Igoma “A”, Kata
ya Isanga, Tarafa ya Sisimba, Jiji na Mkoa wa Mbeya. Jeshi la Polisi
Mkoa wa Mbeya lilipokea taarifa kuwa maiti iliyokwenda kuzikwa katika
makaburini ya zamani ya Isanga kukutwa nyumbani, chumbani ikiwa kwenye
godoro.
Kufuatia taarifa hiyo Polisi walifuatilia na kubaini kuwa tarehe
16.01.2017 majira ya saa 07:00 Asubuhi Mtu mmoja aitwaye JAILO KYANDO
[36] Muosha magari na mke wake aitwaye ANNA ELIEZA [32] wote wakazi wa
Mtaa wa Igoma “A” waliamka asubuhi na kukuta mtoto wao wa kwanza aitwaye
HARUN JAILO KYANDO [09] amefariki dunia akiwa amelala.
Taarifa za awali zinadai kuwa marehemu tangu utoto wake alikuwa na
matatizo ya ugonjwa wa kifafa hali iliyopelekea kuishi nyumbani pasipo
kusoma. Kufuatia kifo hicho msiba uliendeshwa na taratibu za mazishi
zilifanyika. Majira ya saa 12:00 Mchana jeneza lililoletwa msibani na
kuwekwa sebuleni kando ya mwili wa marehemu ambao ulikuwa umeviringishwa
na blanketi na kulazwa chini kwenye godoro, baada ya maombi
yaliyoongozwa na walokole waitwao BONDE LA BARAKA vijana walibeba jeneza
hadi makaburi ya zamani ya Isanga na kisha jeneza kuzikwa.
Waombolezaji waliporudi nyumbani walitaharuki kuona mwili wa marehemu
Mtoto HARUN JAILO KYANDO ukiwa chumbani umelazwa eneo ulipokuwa awali.
Kutokana na hali hiyo taarifa zilifikishwa Polisi mara moja, askari
Polisi walifika na kurejesha hali ya amani kwa kuuchukua mwili wa
marehemu ambao kwa sasa umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.
Taratibu nyingine za mazishi zitafanyika leo tarehe 17.01.2017. Mpaka
sasa bado haijafahamika ni uzembe /bahati mbaya wafiwa kusahau kuweka
mwili wa marehemu kwenye jeneza au kulikuwa na hujuma zozote. Upelelezi
unaendelea kuhusiana na tukio hili.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefika eneo la makaburi alipozikwa
marehemu na kuongoza usimamizi wa ufukuaji wa kaburi hilo ulioanza
majira ya saa Nne na nusu asubuhi hadi saa tano asubuhi.
Baada ya kumaliza kulifukua kaburi hilo vijana walilitoa jeneza kaburini
ndipo Mwenyekiti wa Mtaa wa Igoma A, Fred Mwaiswelo alipofunua jeneza
na kukuta ndani kukiwa tupu hali iliyoashiria mwili wa marehemu
haukuwekwa ndani ya jeneza.
Kutokana na hali hiyo Jeshi la Polisi lilibeba jeneza hilo na kuelekea
nalo katika kituo cha Polisi kati kwa ajili ya uchunguzi zaidi kabla ya
kuwakabidhi ndugu kuendelea na taratibu za mazishi kwa mara nyine.
Hata hivyo baadhi ya ndugu na majirani wa Mtaa wa Igoma wamesema tukio
hilo linaweza kuwa na sura mbili kwa maana hujuma kufanywa kwa maksudi
au bahati mbaya ya kuusahau mwili wa marehemu.
Wamesema inaweza kuwa hujuma kutokana na kawaida ya misiba kabla ya
mazishi lazima ndugu watoe heshima za mwisho kwa marehemu lakini kwa
msiba huo haikufanyika pamoja na baadhi ya ndugu kutohudhuria mazishi ya
marehemu
Today Deal $50 Off : https://goo.gl/efW8Ef
Today Deal $50 Off : https://goo.gl/efW8Ef

No comments