WAJUMBE 14 WA BODI YA KIWANDA CHA MAZIWA CHA AYALABE WAFIKISHWA MAHAKAMANI



Na. Vero Ignatus ,Arusha
 
Wajumbe  14  wa bodi ya kiwanda cha maziwa cha Ayalabe na Saccos willaya ya Karatu wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha zaidi ya shilingi za Kitanzania  607milioni


Wakisomewa mashtaka mbele ya hakimu mkazi mkoa wa Arusha Doroth Msofe pamoja na waendesha mashtaka ,mawakili wa serikali waandamizi Agnessna Halili Nuda,wakati huo washtakiwa wakiwakilishwa na mawakili wasomi Gwankisa Sambo,na mwenzake .


Hakimu aliyekuwa aliyekuwa anaisikiliza kesi hiyo alisema kuwa washtakiwa  hawaruhusiwi kujibu chochote kwa kuwa mahakama yake haina uwezo,


Naye wakili msomi upande wa jamhuri Agness alisema kuwa mahakama hiyo haiwezi kuruhusu dhamana hadi hapo Watakapata mwongozo wa kisheria kutoka kwa mkurugenzi wa mashtaka ,  mahakama hiyo itapata mwongozo kutoka mahakama ya juu (High court)


Ameyataja majina ya watuhumiwa hao  Yuda Morata Male ,Anastazia Morata,Eustela Kastuli Hhyrang,Tarsila Ninah Sule,Ludovic Hunki Marmo,Maria Lohai,Suleiman Mohamed ,Everist Kwaslema,Israel Sarwat, Lazaro Titu, Florence Nesto,Constancy Nina,Saimon Philip, Zulpher Aban,Mohamed Issa ,Dickson Charles 

 Watuhumiwa wote 14 wamepelekwa gereza kuu la Arusha hadi tarehe 9 februari 2017.  

No comments