MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2016 NA DARASA LA NNE YAMETANGAZWA,TAZAMA HAPA
Baraza
la Mitihani nchini – NECTA limetoa matokeo ya mitihani ya upimaji kwa
wanafunzi wa darasa la nne kwa shule zote za msingi nchini pamoja na ule
wa kidato cha pili kwa wanafunzi wa shule za sekondari yanayoonesha
ufaulu kuongezeka kwa 1.9%.
Katibu
Mtendaji wa Baraza lza Mitihani nchini Dkt Charles Msonde ndiye
aliyetoa taarifa hiyo jana jijini Dar es Salaam ambapo katika hali isiyo
ya kawaida, shule tisa kati ya kumi zilizofanya vibaya katika mtihani
wa kidato cha pili nchini, zimetoka mkoani Mtwara kama zinavyoonekana
hapa
Amesema ufaulu umeongezeka kwa asilimia 1.9 kutoka 89.12% mwaka 2015
hadi kufikia 91.02% mwaka 2016 ambapo wanafunzi 372,228 wamepata alama
zinazowawezesha kuingia kidato cha tatu huku wanafunzi 36,737
wakishindwa kufikisha alama hizo.
Shule ya St. Francis Girls ya Mbeya imeongoza katika shule 10 bora
kitaifa katika matokeo ya mtihani wa kidato cha pili mwaka 2016
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, idadi ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri
wa madaraja ya I, II, na III ni 178,115 sawa na asilimia 43.55
Kuhusu ufaulu wa masomo, amesema, katika masomo ya Civics, History,
Geography, Kiswahili, Phiysics, Chemistry, Chemistry, Biology na Basic
Mathematics umepanda ikilinganishwa na mwaka 2015.
Aidha ufaulu kwa somo la English Language pekee ndio ambao umeshuka ikilinganishwa na mwaka 2015.
Somo lililofanyika vizuri zaidi ni Kiswahili ambapo asilimia 90.06 ya
wanafunzi wote, wamefaulu na soko lenye ufaulu wa chini zaidi ni Basic
Mathematics ambapo asilimia 21.55 wamefaulu.
Mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi ni Teckla Erasmo Haule kutoka Canosa
ya Dar es Salaam akifuatiwa na Joseph Fabian Kalabwe wa Kwema Modern ya
Shinyanga na Mirable Rayner Matowo wa Canosa ya Dar es Salaam.
Katika wanafunzi 10 bora kitaifa, wanafunzi 9 ni wasichana, na watano kati yao wanatoka Feza Girls.
Matokeo ya wanafunzi 31 yamefutwa baada ya kubainika kuwa walifanya udanganyifu

No comments