MWAKYEMBE ATEMBELEA MAHAKAMA MAALUM YA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI
Waziri
wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akiangalia chumba
cha kuendeshea kesi katika mahakama ya makosa ya rushwa na uhujumi
uchumi alipoitembelea leo
Waziri
wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akiangalia chumba
cha kuendeshea kesi katika mahakama ya makosa ya rushwa na uhujumi
uchumi alipoitembelea leo
Waziri
wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akimsikiliza kaimu
mkuu wa mahakama hiyo Kanda ya Dar es Salaam Mhe. Jaji Winnie Koroso
alipokuwa akiatoa taarifa ya utendaji wa mahakama hiyo alipoitembelea
leo
Waziri
wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza baada
ya kufanya ziara katika Mahakama malum ya makosa ya Rushwa na Uhujumu
uchumi Kanda ya Dar es Salaam leo
Waziri
wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akiangalia kitabu
ambacho huingizwa orodha ya mashauri yaliyofunguliwa katika Mahakama
maalum ya makosa ya rushwa na ufisadi alipoitembelea leo.
Waziri
wa mambo ya katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe ametembelea
Divisheni Maalum ya Mahakama inayojishughulisha na makosa ya rushwa na
uhujumu uchumi nchini Kanda ya Dar es Salaam na kujionea namna
inavyoendesha shughuli zake.
Akizungumza
katika ziara hiyo Waziri Dkt Mwakyembe amewataka watendaji wa mahakama
hiyo kuzingatia lengo la uanzishwaji wa mahakama hiyo ili kuleta tija na
ufanisi uliofanywa kuanzishwa kwake.
“Mahakama
hii ni chombo maalum kilichoundwa ili kushughulikia masuala ya rushwa
na uhujumu uchumi ndani ya muda mfupi, nyinyi kama watendaji hamna budi
kuongeza bidii na kuhakikisha mashauri yote yanayoletwa katika mahakama
hii yanamalizika ndani ya muda mfupi huku mkizingatia haki za kila mmoja
na hivyo kufanikisha lengo la kuanzishwa kwake ”,alisema Dkt Mwakyembe
Aidha
alisema uanzishwaji wa mahakama hiyo ulilenga kuifanya Tanzania
kupunguza utendaji wa makosa ya aina hiyo au kuyamaliza kabisa na
kuongeza kuwa kwa hali ilivyo sasa inaonekana kuwa uhalifu wa aina hiyo
umepungua.
Kutokana
na kupungua kwa makosa hayo mhe. Waziri alisema anafikiria kuandaa
mpango wa kupunguza kiwango cha gharama za makosa ambayo yatapelekwa
mbele ya mahakama hiyo . “Inaonekana yale makosa ya ufisadi mkubwa
hakuna kwa sasa na hili no moja ya lengo la kunazisha mahakama hii na
kwa hali hiyo nafikiria kuja na mpango wa kupunguza kiwango cha thamani
ya makosa ambayo kitakuwa ni chini ya kile kilichowekwa awali cha sh.
Bilioni moja,” alisema Dr. Mwakyembe.
Akizungumza
katika kikao hicho Kaimu Mkuu wa Mahakama hiyo Maalum Mhe. Jaji Winnie
Korosso alisema mahakama hiyo ina uwezo wa kupunguza kiwango cha thamani
ya makosa husika yanayopaswa kupelekwa na kuongeza kuwa mahaklama hiyo
pia inao uwezo wa kusikiliza kesi zote zinazohusiana na nyara za
serikali bila ya kujali thamani yake.
“Mahakama
hii inao uwezo wa kupunguza kiwango cha thamani ya mashitaka
yanayoletwa hapa, pia ijulikane wazi kuwa mashitaka yote yanayohusu
nyara za taifa yanaweza kuletwa katika mahakama hii wakati bila ya
kujali thamani yake,”alisema Mhe. Koroso
Akiongelea
utendaji kazi wa mahakama hiyo Mhe Jaji Koroso alisema mpaka sasa
mahakama hiyo imeshasikiliza maombi ya dhamana tisa ambapo sita
yameshafanyiwa kazi na maombi mengine yanaendelea kushughulikiwa.
Amesema
mahakama hiyo iko katika kanda zote 14 za Mahakama Kuu nchini na hivyo
mashauri yanayostahili kusikilizwa na mahakama hiyo yanaweza kupokelewa
na kusikilizwa nchi nzima kupitia kanda hizo na sio kwam,ba iko Dar es
Salaam pekee.
Aliasema
kwa kuwa mahakama hiyo ni maalum mashauri yanayopelekwa yanatakiwa yawe
yamemalizika ndani ya miezi tisa (9) na hivyo hazina budi kuendeshwa
kwa haraka ili kufanikisha lengo la kusikilizwa kwa haraka na hivyo
kusaidia taifa.
No comments