Kumbe ndoa ya muigizaji Media sio ya ukweli ila Franck azidi kuumia
Wakati picha ikimuonesha muigizaji wa kike wa Burundi Movie Media, akiolewa
na Franck na tetesi ikizagaa kila kona ya mji, kuhusu arusi ya Media
na Franck, baada ya hayo kuna picha nyingine inamuonesha mrembo Media
amenasa ujauzito wa kijana Franck.
Licha ya mpenzi wa Franck kuinadi picha ya mimba na arusi ya muigizaji
huyo mtandaoni, na kusema kuwa Media amemuibia na amekuja kuaribu
mapenzi yake na Franck.
Media ameibuka na kudai kuwa picha zote zikimuonesha kuwa ameolewa na
akiwa na ujauzito sio ukweli kama wanavyojua na huyo mpenzi wa Franck
bali ni filamu walio wakiigiza mkoani Bubanza, kwa mujibu wa Media
amesema kuwa ukweli utajulikana soon na mtu wa kwanza kushuhudia filamu
hiyo itakapo toka ni mpenzi wa Franck.
Tuwafahamishe kuwa usiano kati ya Franck na mpenzi wake sio nzuri baada
ya picha hizo kuzagaa mtandaoni huku mpenzi wa Franck akidai kuwa
ameibiwa bali kwa mujibu ya Media amesema kuwa ni filamu walikua
wakiigiza na soon itakuwa sokoni.


No comments