DC WA IRINGA,RICHARD KASESELA AMTIMUA MHANDISI RAYMOND SWAI ANAEJENGA MRADI WA DARAJA LA TAGAMENDA
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela(kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Dr. William Mafwele, mwenye miwani ni mhandisi wa Manispaa, Eng. Lihamba .
Mkuu
wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela leo alitembelea mradi wa ujenzi
wa daraja la Tagamenda linalofadhiriwa na serikali ya Uingereza kupitia
shirika lake la DFID. Wakati wa ziara hiyo aliyoongazana na Mkurugenzi
wa manispaa ya Iringa Dr William Mafwele pamoja na mhandisi wa Manispaa, Eng. Lihamba.
Akipokea
taarifa ya kazi, aliambiwa kuwa Mhandisi msimamizi wa Mradi amekuwa
kikwazo cha utendaji na utekelezaji wa majikumu ikiwemo hata kunyanyasa
wafanyakazi. Ndio maana mradi umekuwa unasua sua.
Mkuu
wa wilaya aliamuru Mhandisi Raymond Swai aondolewe haraka na asikanyage
kabisa eneo la mradi akionekana mita 100 achukuliwe hatua. "
OCD
mtafute haraka Raymond Swai mpe amri amri hii kama anabisha atatakiwa
aondoke Iringa" Alisema Mkuu wa wilaya. Muda huo saa 5 asubuhi bado
Mhandisi huyo alikuwa hajafika kazini kufanya kazi na kupelekea kazi
kutoanza kwa wakati.
Mradi huo wenye thamani wa 5.3 bilioni unatarajiwa kukamilika mwisho wa mwezi wa 3 kama mkandarasi atafuata ratiba.
No comments