WAZIRI MWIJAGE AZINDUA BODI YA MAMLAKA YA MAENDELEO YA BIASHARA TANZANIA
Mhe
Charles Mwijage akimkabidhi vitendea kazi Mhandisi Christopher Chiza
Mwenyekiti mpya wa bodi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Tanzania
baada ya uzinduzi wa bodi hiyo
Mhe
Charles Mwijage, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji asisitiza
mageuzi ya kiuchumi kwa maendeleo ya watu yanayolenga katika kujenga
viwanda na kupunguza biashara ya kuuza malighafi na ilenge kwenye
kuhamasisha biashara za kuuza bidhaa zilizoongezwa thamani.
Hayo
aliyasema kwenye uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maendelo
ya Biashara Tanzania (TanTrade) uliofanyika tarehe 16 Januari, 2017
katika ofisi za TanTrade zilizopo kwenye kiwanja cha Mwl J.K Nyerere
barabara ya Kilwa.
Mhe
Mwijage amesema kuwa kazi kubwa ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara
Tanzania (TanTrade) ni kuhamasisha shughuli za biashara Tanzania na
wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji ni wizara ambayo matumaini mengi
ya watanzania yameangalia huko hivyo watu wanategemea matumaini makubwa
sana.
Akaendelea
kwa kusema kuwa kwa mwaka 2017 kwenye maonesho ya 41 ya kimataifa ya
biashara ya Dar es Salaam (DITF) yawe ya tofauti kwa watakaokuja
kuonyesha bidhaa zao kutoka nchi za nje, waoneshaji hao waje na mashine
za viwanda vidogo ili watanzania watakaokuja kuona na kununua mashine
hizo ziweze kusaidia kuongeza thamani za bidhaa zao ili kasi ya kuuza
malighafi nje ya nchi ipungue bali bidhaa za viwandani ziweze kuongezewa
thamani ili kuweza kuuza nje ya nchi.
Mhe
Mwijage aliendelea kuiambia Bodi ya Wakurugenzi iliyoteuliwa kuwa kazi
zote ambazo zilisimama zifanyiwe kazi mapema ili kueza kukamilisha
maamuzi yote usiku na mchana akaongeza kwa kusema kuwa maamuzi ambayo
hayakufanyika ni mabaya mno na gharama zake ni kubwa afadhali maamuzi
ambayo yamefanyika ila mabaya hivyo asingependa kufanya maamuzi ya bodi
bila bodi kumshauri ili aweze kufanya kazi yake kwa ufanisi.
Akaongeza
kwa kusema kuwa tunapoelekea kwenye uchumi wa viwanda Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) yapaswa kwenda kuwafundisha
watanzania ili waelewe kile wanachopaswa kwenda kukiuza nchi za nje na
kuwashawishi wale wanaokuja kuonesha bidhaa zao nchini waje kuonesha
vitu gani kwetu vyenye tija. Natamani maonesho ya kimataifa ya biashara
Dar es salaam (DITF) kuwe na viwanda vidogovidogo vingi, tuwashawishi
wanaokuja kuonesha kwa kutumia teknolojia zao ila yatupasa
kufanyaTantrade kutumia mwenyekiti wao wafanye survey kwa kuhusisha
wataalam kama teknolojia zao zinakidhi haja ya mazingira ya nchi yetu na
matakwa ya wananchi.
Mhe
Mwijahe akatoa maagizo kwa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania
(TanTrade) kuulizia ofisi zote za serikali na za watu binafsi ni
maonesho gani yaliyopo mwaka 2017 sababu kisheria maonesho yote Tanzania
yanasimamiwa na tantrade hata wanaokwenda nje ya nchi kwenye maonesho
mbalimbali wapate Baraka za TanTrade kwa kutambulika hivyo asionekane
asionekane mtu anaenda bila kupata kibali kupitia TanTrade na pia
kuhakikisha taasisi hiyo haitawanyi rasilimali zilizopo bali ikazane
kuongeza trade volume za bidhaa za viwanda ziende kwa wingi nje ya
nchi.
Nae
mhe Mhandisi Christopher Chiza Mwenyekiti wa bodi mpya ya wakurugenzi
kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) alisema kuwa
nguzo kubwa atakayotumia katika kutekeleza majukumu ni sheria
iliyoanzisha mamlaka ya kuendeleza Biashara Tanzania ya mwaka 2009 na
sheria zingine za nchi.
Akaendelea
kusema kuwa kwa uchache majukumu ambayo atakayosimamia ni pamoja na
kusimamia na kujiridhisha kwamba mali za mamlaka zinazohamishika na
zisizohamishika zinatunzwa na zinatumika vzuri kwa manufaa ya Umma,
Kuelekeza mamlaka kubuni na kutafuta vyanzo mbalimbali vya fedha na kwa
fedha zote zitatumika kwa manufaa ya umma, kusaidia mamlaka kubuni na
kubaini fursa za biashara na kuziunganisha fursa hizo na wadau
mbalimbali ili zijulikane ndani na nje ya nchi kuwawezesha wadau wengine
wazichangamkie. Hivyo kama taasisi ya muungano ambayo sehemu kubwa
inawagusa makundi mbalimbali ya wazalishaji hawana budi kupanua wigo wa
huduma hizo ilikuwafikia kwa ukaribu.
Mnamo
Desemba 17, 2016 Mhe Dkt John Magufuli Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania alifanya uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka
ya Maendeleo ya Biashara Tanzania na kumteua Mhandisi Christopher
Kajolo Chiza kuwa mwenyekiti wa Bodi hiyo na kufuatiwa uteuzi wa wajumbe
wa bodi hiyo uliofanywa na Mhe Charles Mwijage Waziri wa Viwanda
Biashara na Uwekezaji.
No comments