WAWILI WAUAWA KWA KUCHOMWA MOTO KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo Afisa Mtendaji wa kijiji cha Ifumbo Emily Rajab
amesema waliouawa wametambuliwa kwa majina ya Paschaly Paul Simchimba
mkazi wa Ileya Lupa Market na Tegemeo Henus mkazi wa Mjele ambapo waliouawa na wananchi waliamua kujichukulia sheria mkononi walipokuwa wakichukuliwa maelezo katika ofisi ya mtendaji.
Rajabu
amesema alitoa taarifa kituo cha Polisi Chunya lakini wakati
wakimsubiri kufika wananchi walimtimua Mwenyekiti wa kijiji na yeye
kisha kuwafunga kamba majambazi hayo na kuanza kuwapiga kwa silaha
mbalimbali kisha kuwachoma kwa kutumia magurudumu ya gari. Polisi
walifika walikuta miili imeteketea kabisa.
Uchunguzi
wa awali umeonesha marehemu walikuwa wamehukumiwa kifungo cha miaka
thelathini jela mwaka 2014 kwa tuhuma za ujambazi wa kutumia silaha na
kusababisha mauaji eneo la Lupa Market ambapo baadaye walitoka.
Kwa
upande wake mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa amesikitishwa na
tukio hilo ambalo limetokea Ifumbo na kuwataka wananchi kuacha tabia za
kujichukulia sheria mkononi kwani wangefikishwa Polisi wangesaidia
kubaini mtandao wa ujambazi.
Baadhi
ya ndugu walionekana eneo la tukio wakishuhudia mauaji hayo ambapo
Polisi walipofika walichunguza na kuamuru kuzikwa miili hiyo kutokana na
kuharibika vibaya .Hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio
hilo.
MBEYA YETU
No comments