WATOTO 22 WAZALIWA MKESHA WA MWAKA MPYA 2017 MORO, WANAUME WAZIDI KUZALIWA


Mkazi wa Mafisa Manispaa ya Morogoro, Vailety Paul (21) akiwa amelala na kichanga chake baada ya kujifungua kwa njia ya upasuaji katika hospitali ya mkoa huo katika mkesha wa mwaka mpya 2017 ambapo jumla ya watoto 22 walizaliwa.


Juma Mtanda, Morogoro.

Jumla ya watoto wachanga 22 wamezaliwa katika mkesha wa mwaka mpya 2017 baada ya wazazi wao kujifungua katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.

Akizungumza na MTANDA BLOG mjini hapa, Muuguzi wa zamu wa hospitali ya rufaa ya mkoa huo, Nelly Nswila alisema kuwa akinamama 22 wamejifungua vichanga 22 katika mkesha wa sikukuu ya mwaka mpya 2017 na hali zao zzinaendelea vizuri.

Nelly alisema kuwa kati ya watoto hao, wakiume ni 13 na kike tisa na wazazi watatu walijifungua kwa njia ya upasuaji baada ya kushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida kutokana na sababu mbalimbali.

“Vichanga 22 vimezaliwa katika mkesha wa mwaka mpya katika hospitali yetu ya mkoa na kati yao watoto wa kiume ni 13 na kike tisa lakini akinamama watatu walilazimika kujifungua vichanga vyao kwa njia ya upasuaji baada ya kushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida hali iliyowalazimi madaktari kuwafanyia wajifungue kwa upasuaji.”alisema Nelly.

Nelly alisema kuwa watoto hao 22 ni idadi ndogo ukilinganisha na idadi ya watoto waliozaliwa katika sikukuu ya krismasi ambapo watoto 25 walizaliwa.

“Sikukuu ya krismasi tunaweza kusema tulipata neema zaidi kwani watoto 25 walizaliwa tofauti na hii ya mwaka mpya watoto 22 ndio wamezaliwa ikiwa ni pungufu ya watoto watatu lakini yote ni neema ya mwenyezi mungu kwani yeye ndiye anayepanga.”alisema Nelly.

Aliongeza kwa kusema kuwa hali za akinamama hao na watoto wao zinaendelea vizuri na muda wowote wataruhusiwa kwenda kulea vichanga vyao manyumbani kwako.

Katika mkesha wa sikukuu ya krismasi jumla ya watoto 25 walizaliwa katika hospitali huku watoto wa kiume wakaiwa 14 na kike 11.

 


No comments