Mwenye
t shirt ya damu ya mzee ni Pius Malindisa ambaye ni mdogo wake marehemu
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio lilivyotokea katika
kijiji hicho.Nyumbani kwa kwa marehemu Atanas Patrick watu wakiwa wamejitokeza kwa ajili ya kwenda kumstili.
JESHI
la polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Patrick Malindisa (29) makazi wa
mtaa wa Namanyigu kata ya Mshangano Manispaa ya Songea mkoani humo
kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi Atanasi Malindisa (70) kwa kumpiga
na kitu chenye ncha butu kichwani na kidevuni upande wa kushoto kisha
kufanya jaribio la kuchimba shimo kwenye nyumba hiyo kwa malengo ya
kumzikia baba huyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika eneo la tukio mmoja wa wanafamilia ambaye ni mdogo
wa marehemu Piusi Malindisa alisema kuwa wao walipata taarifa ya kifo
cha ndugu yao Januari Mosi mwaka huu majira ya 1.30 kutoka kwa mtoto wa
marehemu Patrck Malindisa .
Piusi
alisema kuwa mtoto huyo ambaye alikuwa akiishi kwenye nyumba hiyo na
marehemu huyo alitoa taarifa kwa wanandugu kuwa baba yake amefariki kwa
homa ya tumbo na ndugu walipofika kabla ya kuingia chumbani alikokuwa
akilala marehemu waliamua kuuita uongozi wa mtaa ambao uliingia na
kubaini kuwa Atanasi Malindisa ameuwawa kwa kupigwa na kitu kichwani na
kidevuni.
Alisema
kuwa baada ya kubaini hilo walitoa taarifa polisi kisha mwili huo
ulichukuliwa na kwenda kuuhifadhi Hospital ya mkoa Ruvuma [HOMSO] kwa
uchunguzi huku jeshi la polisi likimshikilia mtoto wa marehemu kwa
mahojiano zaidi.
Alifafanu
kuwa polisi wakiwa bado kwenye nyumba hiyo walibaini kuwa kwenye moja
ya chumba ambacho hakijaezekwa kulichimbwa shimo linaloendana na vipimo
vya marehemu ambalo lilihisiwa kuwa alitaka amfukie humo ili watu
wasijue kwa kuwa kwenye nyumba hiyo walikuwa wakiishi wawili.
“Uchimbaji
wa shimo hilo lenye mithiri ya kaburi lilimshinda kisha akamua
kulifukia na kuchukua hatua ya kuja kutoa taarifa kwetu wanandugu kuwa
baba yake amefariki kwa homa ya tumbo ambayo inadaiwa alikuwa akilia
nalo kumbe sivyo bali kapigwa na kitu kichwani”alisema Ndugu wa
marehemu.
Kwa
upande wake jirani wa nyumba hiyo ambaye hakutaka kulitaja jina lake
alisema kuwa maisha ya marehemu na mtoto wake walikuwa wakipigana mara
kwa mara hasa kwa kutumia silaha na majirani walikuwa hawapo karibu nao
kutokana na tabia hizo.
Vituko
vya tawala kwenye makaburi ya Namanyigu wakati wa uchimbaji wa kaburi
la kumzikia marehemu Atanasi Malindisa ambako mtandao huu umeshuhudiwa
vijana walitaka kugomea kuchimba kaburi hilo kwa madai kuwa familia hiyo
ilikuwa haijihusishi kwenye matatizo ya majirani.
Baadhi ya wazee waliwasii vijana hao kwa kuwaomba wasilipe ubaya kwa
ubaya cha msingi wafanikishe kumuhifadhi marehemu kwa kuwa marehemu
hayupo duniani hivyo ni vema wakasamehe na kumuachia Mungu.
Katika usafirisaji wa mwili huo kutoka katika Hospital ulikohifadhiwa
baada ya magari ya maeneo hayo kutokuonyesha nia ya kutoa msaada gari la
Mbunge wa jimbo la Songea mjini Leonidas Gama ambalo alilitoa kwa
wananchi kwaajili ya matatizo mbalimbali la okoa jahazi kwa kuubeba
mwili wa marehemu huyo.
Naye kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Zuberi Mwombeji amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo pamoja na kumshikilia mtuhumiwa Patrick Malindisa
mtoto wa marehemu na kuwa jeshi hilo linaendelea na upelelezi likiwemo
shimo lililokutwa.
Serikali: Mafuta Yanatosha Hadi Siku 91
-
Serikali kupitia Wizara ya Nishati imeeleza kuwa hali ya upatikanaji wa
mafuta nchini bado ni shwari, huku bei zikiwa himilivu, ambapo mafuta
yaliyopo yana...
WAKALA WA VIPIMO WADHAMIRIA KUTOKOMEZA LUMBESA
-
*Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Vipimo (WMA)
wakiimba wimbo wa ‘Mshikamano Daima’ kabla ya kuanza kikao cha 37 cha
Baraza hilo, k...
No comments