TAARIFA YA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA KUHUSU SIKUKUU ZA KRISMAS NA MWAKA MPYA KWA WANANCHI.
TAARIFA YA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA KUHUSU SIKUKUU ZA KRISMAS NA MWAKA MPYA KWA WANANCHI.
Kama ilivyo desturi tunapoelekea kufunga mwaka, kunakuwa na shamra shamra za wananchi kufurahia na kuona wanavuka mwaka huu na kuingia mpya wakiwa salama.
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo amewahakikishia wananchi wote na wageni watakaotembelea Arusha kuwa jeshi la polisi limejipanga vyema kuhakikisha sherehe hizo zinasherekewa kwa Amani Na utulivu na kwamba wasiwe Na hofu ya ulinzi Wao pamoja na Mali zao.
Katika kuimarisha ulinzi jeshi la polisi mkoani Arusha linatoa onyo kwa watu wachache, kwa baadhi yao wanaopenda kuvuruga Amani na utulivu tulionao kwa kujiingiza katika uhalifu, tunawataka waache Mara moja kujiingiza katika fikra hizo, Hatutasuta kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wote ambao watakaobainika kujihusisha Na matukio ya kihalifu.
Pia katika kuimarisha ulinzi Na usalama, jeshi la polisi linakataza uchomaji wa matairi barabarani tunapoukaribisha mwaka mpya.
Aidha amewataka wafanyabiashara wa vileo na majumba ya starehe wafuate masharti ya leseni zao , na pia amepiga marufuku kuwapeleka watoto kwenye majumba ya starehe na vileo Na kusema kuwa huo sio utamaduni nzuri kwa malezi ya watoto.
Ni marufuku kuendesha gari dereva akiwa amelewa au anaendesha kwa mwendo Kasi barabarani kwani hatua kali zitachukuliwa dhidi yai.
Kamanda amewataka wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kuwabaini Na kufichua watu wachache wenye nia ovu ya kihalifu tunapoelekea kusheherekea sikukuu hizo za krismas Na mwaka mpya kutoa taarifa zao waweze kuchukuliwa hatua za kisheria Ili kuzuia uhalifu usitokee.
No comments