BLOGGERS WATAKIWA KUIKOSOA SERIKALI ILI KUIPATA TANZANIA INAYOTAKIWA


Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wakati wa ufungaji wa wa mafunzo kwa mablooger Tanzania yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Muda wa Tanzania Bloggers network Bw. Joachim Mushi akizungumza na wamiliki wa Bloggers Tanzania kabla ya kumkaribisha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye kufunga mafunzo kwa Bloggers Tanzania yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.



Na. Vero Ignatus, Dar es salaam
Waziri wa habari mhe,Nape Nauye amesema kuwa serikali inatambua na kuthamini mchango wa waandishi wa habari za mtandaoni (BLOGGERS)kwani wanayo nguvu kubwa ya kuwafikishia jamii habari kwa haraka zaidi kuliko chombo chochote kile cha habari.
Ameyasema hayo wakati akifunga mkutano wa mafunzo wa siku mblili wa Tanzania Bloggers uliofanyika jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Golden Jubilee katika jengo la PSPF - Dar es Salaam.
Nape amewataka waandishi wa habari za mtandaoni kuikosoa serikali kwa kufuata maadili hadi pale watakapoipata Tanzania wanayoitaka.
"Ikosoeni serikali kwa kadri mnavyoweza ili tuweze kuipata Tanzania tunayoitaka, kwani nyie huwa mnaweza kuturahisishia kazi na sekta(bloggers) hii ndiyo yenye nguvu zaidi nchini na nje ya nchi".
Wakati huohuo waziri wa habari amesema kuwa serikali kwa kushirikiana na Tanzania Bloggers Network(TBN) kuna haja ya kuanzisha Tuzo za Bloggers nchini ilikuleta ufanisi katika kazi zao.
No comments