
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim
Majaliwa(kushoto)akipokea mfano wa hundi wenye thamani ya Tsh Milioni 20
kutoka kwa Meneja wa TIB Corperate Bank Limited tawi la Arusha, Bi.
Juliana Mwansuva (kulia) ukiwa ni mchango wa benki hiyo kwa ajili ya
kununua Pikipiki ambazo Waziri Mkuu amezikabidhi leo kwenye uwanja wa
Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha wanaoshudia kutoka kushoto ni Mkuu wa
mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo, Mkurugenzi Mkuu wa TIB Corperate Bank, Bw.
Frank Nyabundege na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne
Maghembe.

Meneja
wa TIB Corperate Bank Limited tawi la Arusha,Juliana
Mwansuva(kulia)akipongezwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo baada
ya kumkabidhi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Mheshimiwa Kassim Majaliwa(kushoto) mfano wa hundi wenye
thamani ya Sh 20 milioni kwaajili ya kununua Pikipiki .

Baadhi
ya walionufaika na Pikipiki zilizotolewa na Waziri Mkuu ambazo
zilichangiwa na wadau mbalimbali mkoani Arusha. Mradi huo utawawezesha
vijana kurejesha fedha zenye thamani ya Pikipiki kisha kuwa wamiliki
halali.

Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa na Mkuu
wa mkoa wa Arusha, Me. Mrisho Gambo wakizungumza na mmoja wa watu
wenye ulemavu walionufaika na msaada wa Pikipiki leo.

Pikipiki
mpya zaidi ya 200 zenye thamani ya Sh 400 milioni zilizotolewa kwa
vijana jijini Arusha leo katika ziara ya Waziri Mkuu,Kassim
Majaliwa.
No comments