Ujauzito hubadilisha ubongo wa mwanamke
Wanasayansi wanasema kuwa mjamzito hubadilisha ubongo wa mwanamke, kwa kipindi cha hadi miaka miwili.
Uchunguzi ulifanyiwa wanawake 25 waliokuwa wameshika mimba kwa mara ya kwanza ulionyesha mabadiliko hayo kwenye ubongo hudumu kwa hadi miaka miwili baada ya mwanamke kujifungua.
Watafti hao wanasema vipimo vya sehemu tofauti za ubongo hubadilika kipindi hicho, sawa na inavyofanyika mtu anapovunja ungo.
Lakini hata hivyo, hawakupata ushahidi wowote wa kuathirika kwa uwezo wa mwanamke kuweka kumbukumbu.
Wanawake wengi husema huwa wanajihisi kuwa wasahaulivu na kuwa wepesi wa kuekwa na hisia wakati wanabeba mimba.
Mara nyingi huwa wanalaumu kilichobandikwa kuwa ubongo wa "uja uzito" au "mtoto".
Ongezeko la homoni
Mwanamke anapokuwa na mimba, kiwango cha homoni ya oestrogen huongezekana sana na pia mwili wake kubadilika, watafiti wanasema.Hata hivyo, si wataalamu wengi walikuwa wamechunguza mabadiliko kwenye ubongo.
Watoto kuzaliwa na wazazi watatu Uingereza
Watafiti kutoka vyuo vikuu vya Universitat Autonoma de Barcelona na Leiden walichunguza ubongo wa wanawake kabla ya kushika mimba, muda mfupi baada ya kujifungua na miaka miwili baadaye kuangalia mabadiliko kwenye ubongo.
Matokeo ya utafiti wao yamechapishwa kwenye jarida la Nature Neuroscience.
Walishuhudia kupungua sana kwa seli za ubongo katika maeneo ambayo hutumiwa na ubongo katika kuhusiana na watu wengine.
Watafiti wanasema mabadiliko hayo huenda ni ya kuwafaa wanawake kwa njia kadhaa zikiwemo - kuwawezesha kupangia mahitaji ya watoto wao, kuwa na ufahamu zaidi kuhusu hatari kwa watoto wao kutoka kwa jamii na pia kuwawezesha kuhusiana zaidi na watoto wao.
No comments