RAIS MAGUFULI AONGOZA MAELFU KTK SHEREHE ZA MIAKA 55 YA UHURU WA TANZANIA BARA:ASEMA RUSHWA NI KANSA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi waliojitokeza katika sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi waliohudhuria  sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama wakati wimbo wa Taifa ulipokuwa ukipigwa uwanjani hapo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride. 

Vikosi mbalimbali vya Majeshi vikipita mbele ya mgeni Rasmi kwa mwendo wa pole na Haraka katika sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Kikosi cha Maadhimisho cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania kikionesha gwaride la kimyakimya mbele ya Amiri Jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Uhuru.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembea pamoja  na  Askari Polisi ambao huongoza misafara ya viongozi VIP riders mara baada ya kuwasili Ikulu wakati wakitokea katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi mara baada ya Kuwasili katika uwanja wa Uhuru.PICHA ZOTE/IKULU

 Na.Vero Ignatus,Dar es salaam

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli amewaongoza watanzania katika kusheherekea maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru wa Tanzani katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es  salaam
 

Dkt Magufuli amesema kuwa siku hii ni siku muhimu sana katika Taifa la Tanzania, amesema ni vyema kuwakumbuka waanziilishi wa chama cha Tanu wakiongozwa na hayatiBaba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere waliojitoa kwa hiari yao wenyewe kuutafuta uhuru wa Tanzania.


Rais amesema changamoto kubwa waliyonayo serikali ni umaskini,pamoja na  wala rushwa ambao serikali inajitahidi kuitatua,huku akisema kuwa hatasita kuwatumbua hadharani waliozowea kutumbua mali za watanzania hadharani,na wananchi mtambue kuwa rushwa ni KANSA


Katika kuadhimisha miaka 55 ya uhuru Tanzania tumepata mafanikio makubwa tumelinda uhuru wa nchi yetu,mipakani,tunafanya mambo yetu wenyewe,Amani na umoja pamoja na mshikamano,na Watanzana wamebakia kuwa wamoja ,hatubaguani rangi, imepiga hatua katika maeneo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara za kisasa,madaraja,vivuko,meli,viwanja vya ndege na miradi ya maendeleo n.k”amesema Magufuli.


Aidha rais amesema kuwa pamoja na kuhakikisha taifa linabana matumizi bado imegundulika kuwa wapo wafanyakazi hewa 19,000,kwenye mradi wa Tasaf zipo kaya masikini hewa 55,000 na wanafunzi hewa 65,000 ,”sintalifumbia macho kwani juhudi zote hizi ni kwaanjili ya  kuboresha maslahi ya watanzania wote na siyo mtu binafsi “alisema Magufuli.


Amewaomba Watanzania waendelee kudumisha Amani,mshikamano na waendelee kuulinda Muungano wa Tanzania,huku akiwatakata Watanzania waendelee kuchapa kazi kwa bidii .”kama falsafa yetu inavyosema’ hapa kazi tu’ huku wakijua kuwa hakuna babu,bibi,shangazi,wala mjomba wa kuiletea maendeleo nchi hii ya Tanzania ila sisi wenyewe”alisisitiza rais.

Wakati huohuo Dkt Magufuli amesema sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya uhuru mwaka 2017 yatafanyika makao makuu ya nchi Dodoma na kusisistiza kuwa kwa jiji la Dar es salaam itakuwa ndiyo ya mara ya mwisho haya ya miaka 55 ya 2016.

No comments