JESHI LA POLISI LAIMARISHA ULiNZI KUELEKEA SIKUKUU ZA MWISHO WA MWAKA

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba
Jeshi la
polisi limesema limeimarisha ulinzi kuelekea sikukuu za Kristimasi na
mwaka mpya hili kudhibiti vitendo vya uharifu .Akizungunza leo, Msemaji
wa Jeshi la Polisi, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Advera
Bulimba amesema jeshi la polisi katika kipindi cha sikukuu kuna watu
wanajipanga kufanya uhalifu hivyo jeshi la polisi litafanya doria za
kutosha.
Amesema kumbi zote zinazofanya starehe za kupiga mziki ziingize watu kutokana na ukumbi na watakaozidisha watachukuliwa hatua.
Afande
Advera amesema wataondesha vyombo vya moto wataobainika wametumia
vilevi watachukuliwa kwani nia yao nikutaka kusababisha ajali.
Aidha
amesema wazazi wanatakiwa kufanya ulinzi kwa watoto wao kutokana na
watoto kupotea katika siku za sikuu na kusababisha vituo vya polisi
kuwepo kwa watoto hao.
Hata hivyo amesema wananchi watoe ushirikiano kwa jeshi la polisi pale wanapohisi kuna watu wanaashiria kufanya uhalifu.
Advera
amesema kuwa wale ambao watatoa taarifa zikashindwa kutekelezeka
wawasiliane na ngazi ya juu ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa watu
waliofanya uzembe.
No comments